Habari za Punde

Wawakilishi wapatiwa semina juu ya muongozo wa mashirikiano baina ya Serikali na washirika wa maendeleo

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid akifungua warsha ya siku moja kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi juu ya muongozo wa mashirikiano baina ya Serikali na washirika wa maendeleo na muongozo wa utafutaji fedha, ruzuku na mikopo kwa miradi ya maendeleo hafla iliyofanyika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla (kulia) akiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Jamali Kasim Ali wakisikiliza hutuba ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid (hayupo pichani) alipokua akifungua warsha kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Afisa mipango muandamizi kutoka Idara ya Mipango Wizara ya Fedha Zanzibar Dr. Ramadhan Khamis Sosela akiwasilisha mada ya utaratibu wa uwaandaaji wa miradi na utafutaji rasilimali fedha wakati wa warsha ya wajumbe wa baraza la wawakilishi iliyofanyika Chukwani.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia mada mbalimbali zilizotolewa na wawasilishaji (hawapo pichani) katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Idara ya Mipango Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia mada mbalimbali zilizotolewa na wawasilishaji (hawapo pichani) katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Idara ya Mipango Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar.

Mwakilishi wa Jimbo la Pangawe Ali Suleiman (mrembo) akichangia kitu katika warsha ya muongozo wa mashirikiano baina ya Serikali na washirika wa maendeleo na muongozo wa utafutaji fedha, ruzuku na mikopo kwa miradi ya maendeleo iliyofanyika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Picha na Makame Mshenga.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.