RAIS wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amezitaka
Halmashauri za Wilaya na Mabaraza ya Miji kutumia vyema fedha wanazokusanya
kwa miradi ya Maendeleo, badala ya
kujikita katika matumizi ya kawaida..
Dk. Mwinyi amesema hayo katika mkutano wa Majumuisho uliofanyika Ukumbi wa Skuli ya Bumbwini, baada ya kukamilisha ziara yake ya siku mbili katika Mkoa wa Kaskazini Unguja, kuangalia shughuli za maendeleo .
Amesema hali ilivyo hivi sasa kwa Halamshauri na Mabaraza ya Miji ndani ya Wilaya za Mkoa huo zinabainisha kuwepo matumizii makubwa ya fedha zinazokusanywa kwa matumizii ya kawaida.
Alisema utaratibu huo unatia mashaka makubwa na unapaswa kuchukuliwa hatua, akabainisha azma yake ya kuchaguwa Wakurugenzi wapya hivi karibuni ili kuondokana na hali hiyo.
Aidha, aliagiza Mifuko ya kuwawezesha wajasiriamali iliopo nchini iweze kutafutiwa njia ya kuunganishwa na kuwa na mtaji mkubwa ili kuweza kutumia dhamana ya serikali kukjopa katika Mabenki na kuwafikia wajasiriamali wengi zaidi,
Alisema pamoja na Zanzibar kuwa nchi kisiwa na kuwa an wavuvi wengi, lakini bado wanafanya shughuli zao kwa kutumia vifaa duni pamoja na kukosa masoko ya kuuzia samaki.
Alisema hatua hiyo inatokana an serikali kushindwa kuwawezesha wavuvi hao kwa kuwapatia Maboti makubwa na ya kisasa yatakayowawezesha kufika mbali na kupata samaki wengi.
Aliiagiza Wizara ya uchumi wa Buluu kujipanga vyema ili kufahamu idadi ya wavuvi, mahitaji yao na misaada wanayohitaji ili hatimae waweze kusaidiwa kupatiwa vyombo vya kisasa pamoja na masoko kwa kuyahamasisha Makampuni makubwa kuja nchini kuwekeza kwenye Viwanda vya kusarifu samaki.
Abdi Shamna, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777476982. Fax: 024
2231822
E-mail: abdya062@gmail.com
No comments:
Post a Comment