Meneja utekelezaji mradi wa Viungo Bi Khadija Juma akitoa maelezo kwa vijana waliofika katika banda hilo.
Muonekano wa banda la mradi wa Viungo katika maonesho ya sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salam
Na Muhammed Khamis
Wananchi wa Jiji la Dar es Salam na maeneo jirani ya Mkoa huo wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika maonesho ya saba saba kwa lengo la kujifunza na kuonegeza uelewa kuhusu utekelezaji wa mradi wa viungo visiwani Zanzibar.
Wito huo umetolea na meneja utekelezaji wa maradi wa viungo kanda ya Unguja Bi Khadija Juma katika maonesha ya saba saba yanayoendelea jijini Dar es Salam.
Alisemea kupitia mradi huo ambao unatekelezwa Zanzibar wananchi watapata kujifunza na kuona bidhaa zinazozalishwa na wakulima ambao ni wanufaika wa mradi huo.
Alieleza kuwa kwa kiasi kikubwa bidhaa ambazo zimeanza kuzalishwa na wanufaika wa mradi huo zimekua bora na zenye kuvutia kwa kila anaefika kwenye banda la maonesho hayo.
Akifafanua zaidi meneja huyo alisema kwa mfano zao la vanila na baadhi ya bidhaa nyengine za viungo zimeonekana kuwa kivutuo kikibwa kwa kila anaefika na kujionea.
Baadhi ya wananchi waliofika katika banda hilo wameonesha kushangazwa kwao na ubora wa bidhaa zinazozalishwa Zanzibar wakisema zina ubora wa kuvutia na zinaweza kufanya vizuri hata katika soko la kimataifa.
Miongoni mwa wananchi hao aliejitambulishwa kwa jina la Jeremiah Sigala alisema bidhaa alizoziona katika banda hilo ni adimu sana na zenye harufu nzuri mno.
Alisema kwa muda mrefu amekua akishuhudia bidhaa zenye mfano wa bidhaa hizo lakini hazifanani kabisa kwa harufu na ubora wake.
Alishauri watekelezaji wa mradi huo kuona ni kwa namna gani wanaweza kusambaza bidhaa hizo nje ya Zanzibar ili wananchi walio wengi waweze kunufaika nazo.
Nae Wema Ngoi kutokea Kibaha alisema amevutiwa sana na elimu alioipata zaidi kilimo cha nyumbani na kuahidi kukifanyia kazi.
Alisema yeye kama mama wa nyumbani asiemiliki eneo kubwa la ardhi lakini amejifunza namna bora ya kuanzisha kilimo ambacho atakifanya ndani ya eneo la nyumba yake ili nayeye awe miongoni mwa akinamama wenye kupata lishe bora ya kila siku.
Mradi huo wa Viungo unatakelezwa katika wilaya 11za Unguja na Pemba utawanufaisha wanufaika zaidi ya elfu 50 kutoka Unguja na Pemba umefadhiliwa na umojwa Ulaya
No comments:
Post a Comment