Habari za Punde

Diwani avipigia chapuo Vikundi vya kukusanya taka katika Wilaya ya Magharibi B

Na Takdir Suweid

 Wilaya ya Magharibi B.


Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii Baraza la Manispaa wilaya ya Magharibi B Thuwaiba Jeni Pandu amevitaka vikundi vya usafi kujitahidi kufanya kazi kwa bidii ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kutilia mkazo suala la  usafi.

Ameyasema hayo huko kwa mchina mwanzo wakati alipokuwa Akizungumza na vikundi vya kukusanya taka katika wilaya ya magjaribi B.

Amesema malengo ya baraza hilo ni kuzikusanya na kuzisarifu taka hizo na kuweza kuwa mkaa,mbolea na vyombo vyengine vya plastic.

Amewataka Wafanyabiashara na wananchi kushirikiana na vikundi hivyo ili kuwawezesha kufanya kazi kwa ufanisi na kufikia malengo yaliokusudiwa.

Hata hivyo amewataka wananchi kulipia ada ya taka ili iweze kurudi kusaidia jamii katika masula ya maji,njia za ndani,huduma za afya na elimu.

Nao wanavikundi vya ukusanyaji wa taka katika wilaya ya Magharibi B wamesema wanakabiliwa na tatizo la uhaba wa magari ya kukusanyia taka,kukosa mikataba mipya ,vifaa na vituo maalum vya kukusanya taka.

Hivyo wameiomba baraza Hilo kuwatatulia matatizo hayo ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na kuepukana na lawama mitaani.

Zoezi la Mradi mpya wa ukusanyaji taka katika Wilaya ya Magharibi B linatarajia  kuanza kwa majaribio katika shehia ya Uzi,Taveta na Pangawe.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.