Habari za Punde

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Imetakiwa Kutafuta Wakarandasi Wenye Uwezo -Kamati ya BLW.

Na Maaulid Yussuf WEMA  ZANZIBAR

Kamati ya Ustawi wa jamii ya Baraza la Wawakilishi, Imeitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kuhakikisha  wanatafuta Wakandarasi wenye uwezo na waaminifu katika miradi mikubwa iliyopo ili kuepuka hasara zinazoweza kutokea.

Akizungumza wakati wa kikao cha kuwasilisha ripoti ya utekelezaji wa Mpango wa Elimu kwa kipindi cha robo ya Julai-Septemba 2021/2022 katika ukumbi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Karume, Makamo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe, Mwantatu Mbarak Khamis amesema kumekuepo ubabishaji kwa badhi ya wakndarasi wakati wa ujenzi wa miradi mbali hali inayopelekea kuchelewa kwa ujenzi wa majengo kwa mujibu wa mkataba ulivyokusudiwa.

Pia ameitaka Wizara kuwa na umakini kwa Wakandarasi kwa  kuepuka gharama kubwa hasa wanapojenga miundombinu hiyo katika maeneo ya visiwa pamoja na kuwa makini katika ufuatiliaji wa miradi hiyo kwa ukaribu zaidi.

Hata hivyo Wameitaka Wizara ya Elimu kuwasimamia Walimu katika utendaji wao wa kazi ili kupunguza tatizo la kufeli kwa  Wanafunzi, pamoja na kuwafuatilia katika mahudhurio yao, kwani utoro wa Wanafunzi unaweza kuchangiwa na utoro wa Mwalimu.

Hata hivyo kamati hiyo, imeipongeza Wizara ya Elimu kwa kuyapa nguvu Mafunzo ya Amali, na kuwataka kupapanga mikakati ya kuiendeleza Taasisi ya Karume katika kuimarisha Miundombinu ya Majengo  kutokana na vifaa walivyonavyo wanakosa pahala pa kuvihifadhi.

Akiwasilisha ripoti ya utekelezaji wa Mpango wa Elimu kwa kipindi cha robo ya Julai-Septemba 2021/2022 , Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe, Simai Mohammed Said amesema Wizara ya Elimu imekusanya jumla ya shilingi milioni 90 laki 6 mia moja na 14 elfu mia 440 ambapo imekiuka shabaha iliyojiwekea ya kukusanya milioni 42, 475,500.

Amesema makusanyo hayo yamekusanywa katika kipindi cha robo mwaka ambapo ongezeko la makusanyo hayo yametokana na ukusanyaji wa chanzo kipya cha mapato ambacho ni malipo  ya mitihani ya Skuli za binafsi pamoja na malipo ya leseni za Walimu na usajili wa Skuli za binafsi.

Mhe, Simai amesema fedha hizo zimetumika katika masula mbalimbali ya kuimarisha masuala ya Elimu katika nyanja mbalimbali.

Amesema pamoja na Wizara hiyo kukusanya fedha hizo lakini bado ina changamoto ya bajeti na hiyo inapelekea kusuasua kwa baadhi ya utekelezaji wa majukumu yake.

Amesema pia Wizara ina changamoto ya msongamano mkubwa wa Wanafunzi darasani hasa elimu ya mandalizi na msingi, uhaba wa walimu hasa wa Sayansi na hesabati, uhaba wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia, matumizi madogo ya teknolojia katika elimu yanayosababishwa na uhaba wa vifaa vya ICT katika Skuli pamoja na uhaba wa wasaidizi wa maabara na wakutubi.

Hata hivyo mhe Simai ameeleza kuwa Wizara ya Elimu, ina miradi mitano yenye lengo la kuhakikisha inafikia malengo yake ikiwemo mradi wa uimarishaji wa Elimu ya Maandalizi na Msingi, Mradi wa uimarishaji wa Elimu ya Msingi, Mradi wa uimarishaji Elimu ya Lazima, mradi wa uimarishaji wa Elimu Mbadala na Amali pamoja na Mradi wa uimarishaji wa miundombinu katika Elimu.

Akizungumzia kuhusu matumizi ya fedha za IMF amesema Wizara imekusudia kujenga Skuli 35 za maandalizi, msingi na Sekondari Kwa unguja na Pemba pamoja na kuzifanyia matengenezo makubwa baadhi ya Skuli, kujenga.nyumba za walimu pamoja na kujenga vyoo.

Nae Katibu Mkuu Wizara hiyo bwana Ali Khamis Juma ameiahidi kamati hiyo kuwa itataekeleza maagizo yote waliyotakiwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.