Habari za Punde

Balozi Seif mgeni rasmi katika ufunguzi wa Chuo Cha Mafunzo Hanyegwa Mchana

Jengo la Chuo cha Mafunzo Hanyegwa Mchana lililofunguliwa na Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu Balozi Seif Ali Idi Hanyegwa Mchana Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja .Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mstaafu Balizi Seif Ali Idi akisalimiana na Makamanda mara baada ya kuwasili katika hafla ya Ufunguzi wa Chuo Cha Mafunzo Hanyegwa Mchana Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja .Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mstaafu Balizi Seif Ali Idi akipiga makofi  mara baada ya kufungua pazia  ikiwa ni Ishara ya  Ufunguzi wa Chuo Cha Mafunzo Hanyegwa Mchana Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja .Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Masoud Ali Muhammed .

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mstaafu Balizi Seif Ali Idi akikata Utepe kuashiri Ufunguzi wa Chuo Cha Mafunzo Hanyegwa Mchana Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja .Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
-Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mstaafu Balozi Seif Ali Idi (katikati)akiwa katika Picha ya Pamoja na Makamanda wa Chuo cha Mafunzo katika Hafla ya Ufunguzi wa Chuo Cha Mafunzo Hanyegwa Mchana Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja .Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Masoud Ali Muhammed .akitoa hotuba ya makaribisho kwa Mgeni Rasmi katika hafla ya Ufunguzi wa Chuo Cha Mafunzo Hanyegwa Mchana Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja .Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mstaafu Balozi Seif Ali Idi akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Chuo Cha Mafunzo Hnyegwa Mchana Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja .Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 

PICH ANA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

 

Na Kijakazi Abdalla         Maelezo 

Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi amewataka wazee kuwalea vijana katika misingi iliyo bora  na sharia ili kuepuka kwenda katika vyuo vya mafunzo.

Aliyasema hayo katika ufunguzi wa Chuo cha Mafunzo Hanyegwamchana Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni miongoni mwa  shamrashamra za kutimiza miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Amesema ni vyema vijana wetu tukawalea watoto  katika misngi iliyo bora pamoja na kutovunja sheria za nchi ili kuepuka kwenda vyuo vya mafunzo.

Aidha amesema jengo hilo ni la kisasa ambalo linakidhi vigezo vyote vya haki za binaadamu za kitaifa na kimataifa lakini si pahala pa kukaa.

Amesema lengo la kufunguliwa jengo hilo la kisasa ambalo lina uwezo wa kuchukua watoto 250 ni shabaha ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuweka vijana wanaotumikia vifungo vyao kwa misingi bora.

Aidha Mheshimiwa Balozi amesema jamii  iwele kwamba vijana ambao wanapokuwa katika vyuo vya mafunzo sio kama wote wanavunja sheria. Kuna wengine wanakuwa watukutu

Hata hivyo ameitaka jamii kutowatenga vijana ambao wametumikia vyuo vya mafunzo kwani kwenda kwao huko ni ehemeu ya kujifunza pale walipokosea.

Akizungumzia suala la udhalilishaji Mheshimiwa Balosi amewataka mahakiku pamoja na Jeshi la Polisi kurahisha kutoka huku ili kuondokaana na mrundukano mahabusu.

Aidha amesema imebaina kuwa kila siku kumekuwepo kwa kesi za udhalilishaji jambo ambalo limekuwa linaitia aibu Serikali.

Nae  Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara za SMZ.Masuod Ali Mohammed amesema kufunguliwa kwa Chuo hicho ni moja ya fikra  Mheshimiwa  Balozi Seif Ali Iddi wakati alivyokuwa madarakani alipotembelea Kinuwa miguu na kuona hali ya mrundukano  wa wanafunzi ndani ya chuo hicho ni sehemu ya mawazo ambayo yaliyowezeshwa kujengwa chuo cha Hanyegwamchana.

Amesema ni wazi kwamba hali hiyo imekuwa ni sehemu ya nchi zilizotuzunguka ndani ya Afrika Mshariki wa ukanda wa janga la sahara kuja kujifunza Zanzibar  inavyotekeleza haki za binadamu.

Mapema Kamishna wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Khamis Bakar Khamis  amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itahakikisha vijana inawajengea uwezo wa kuwapatia maadili mema. 

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.