Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Aendelea na Ziara Yake Pemba na Kuweka Jiwe la Msingi Kituo cha Wafanyabiashara na Wajasiriamali Tumbe.

MUONEKANO wa Milango ya Maduka katika Kituo cha Wafanyabiashara na Wajasiriamali  Tumbe kilichowekwa Jiwe la Msingi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, kikiwa na Milango ya Maduka 54, Majengo Matatu.
Moja ya Majengo Matatu ya Kituo cha Wafanyabiashara na Wajasiriamali wa Tumbe Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba. 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akimsikiliza Mhandisi wa Kampuni ya Ujenzi ya Kikosi cha KMKM S/LT.Khamis Said Mohammed akitowa maelezo ya michero ya Kituo cha Biashara cha Wajasiriamali Tumbe Wilaya ya Micheweni Pemba, na (kulia kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ.Mhe Masoud Ali Mohammed na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe. Salama Mbarouk na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisoma maelezo ya Jiwe la Msingi la Kituo cha Wajasiriamali Tumbe Wilaya ya Micheweni Pemba, baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kituo hicho akiendelea na ziara yake katika Mkoa wa Kaskazini Pemba kutembelea Miradi ya Maendeleo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mkuu wa Kikosi cha KMKM Commodore Azana Hassan Msingiri akitowa maelezo ya Kituo cha Wajasiriamali Tumbe, wakati akitembelea Ujenzi huo baada ya kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi huo, na (kulia kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe Masoud Ali Mohammed.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi akitembelea ujenzi wa Kituo cha Wajasiriamali Tumbe Wilaya ya Micheweni Pemba, baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kituo hicho na (kulia kwa Rais ) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Mkuu wa Kikosi cha KMKM Commodore Azana Hassan Msingiri na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maluum za SMZ Mhe. Masoud Ali Mohammed.
WANANCHI wa Kijiji cha Tumbe Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akizungumza na Wananchi baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kituo cha Wafanyabiashara na Wajasiriamali Tumbe Wilaya ya Micheweni Pemba, wakati wa ziara yake kutembelea Miradi ya Maendeleo katika Mikoa Miwili ya Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.