Habari za Punde

WAZIRI NDALICHAKO: SERIKALI KUJENGA VITUO VITANO VYA KULEA UJUZI WA VIJANA NCHINI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akijaribu kufanya shughuli ya useremala wakati alipofika Chuo cha Ufundi Stadi Don Bosco Dodoma kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi inayoratibiwa na ofisi hiyo, ambapo wanafunzi 276 wanafadhiliwa kwa mwaka 2022. Wengine ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka na Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Jabiri Shekimweri.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema kwa mwaka wa fedha 2022/23, serikali inatarajia kujenga Vituo Atamizi vya kulea ujuzi wa vijana kwenye kanda tano nchini.

 

Vituo hivyo, vitatoa fursa kwa vijana kufanya mafunzo kwa vitendo sambamba na kufanya shughuli za uzalishaji mali kwenye vituo hivyo ili waweze kujiingizia kipato kutokana na ujuzi watakao kuwa wameupata kwenye vituo hivyo.

 

“Kwa mfano ukimaliza mafunzo yako ukitaka kusindika chakula kutakuwa na vifaa ambavyo vinaweza kutumika, na itaongeza fursa kwa vijana hasa wasio na uwezo wa kununua vifaa vya kusindika au kufanya shughuli aliyopata ujuzi,” alisema

 

Mhe. Ndalichako ameyasema hayo tarehe 19 Julai 2022 wakati akizungumza na wanafunzi wa Vyuo vya ufundi vya Don Bosco na VETA jijini Dodoma ambao wananufaika na Programu ya Taifa ya kukuza ujuzi inayotekelezwa na Ofisi hiyo.

 

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan inatekeleza programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi ili kuhakikisha watu wasio na ajira ambao wako katika soko la ajira wanawezeshwa kwa kujengewa ujuzi utakao wasaidia kufanya shughuli za kiuchumi na hatimaye kujiajiri, kuajiriwa ama kuajiri wenzao.

 

Amefafanua kuwa kwa mwaka wa fedha 2022/23 serikali imepanga kuendelea kuongeza wigo wa fursa za ajira kwa kutoa mafunzo ya ujuzi wa uchumi wa bluu kwa maeneo ya maziwa na bahari. Mafunzo hayo yatawezesha katika fani ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba, ambapo thamani ya Samaki na dagaa itaongezwa.

 

Aidha, amesema kupitia programu hiyo katika mwaka wa fedha ulioishia Juni, 2022, serikali imewezesha jumla ya vijana 30,690 kupata ujuzi,

 

“Serikali ilitoa fedha na kuwezesha mafunzo kwa   vijana 3,600 kupata ujuzi wa kilimo cha kisasa kwa kutumia Vitalu Nyumba, Wahitimu wa elimu ya juu 2,246 wamepata mafunzo ya uzoefu wa kazi (internship), Vijana 2,644 wamerasimishiwa ujuzi wao walioupata nje ya mfumo rasmi wa mafunzo, na Vijana 22,200 wamepata ujuzi katika stadi kupitia mafunzo ya Uanagenzi” amesema Waziri Ndalichako.

 

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka, aliwataka vijana hao kuthamini jitihada zinazofanywa na serikali ya kuwakwamua kiuchumi kwa kutoa mafunzo bure ya ujuzi.

 

Awali, Mkuu wa Chuo cha Ufundi Don Bosco, Padri Boniphace Mchami, pamoja na Mkuu wa chuo cha VETA Mwalimu,  Stanslaus Charles, wamesema program hiyo imewawezesha vijana kupata ujuzi wa fani zitakazowasaidia kujiajiri na kuajiriwa.

 

 

Wakiongea kwa nyakati tofauti vijana wanaonufaika na program hiyo katika vyuo hivyo, wameishukuru serikali kwa kufadhili wa kutoa mafunzo katika fani tofauti kwa vijana ambao wengi walikuwa majumbani na hawakuwa na shughuli za kuwaingizia kipato.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akifuatilia shughuli za mafunzo ya ufundi stadi wanayopata wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi Don Bosco Dodoma chini ya ufadhili wa Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi inayoratibiwa na Ofisi hiyo wakati alipofuatilia utekelezaji wake
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akifuatilia shughuli za mafunzo ya ufundi stadi wanayopata wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi Don Bosco Dodoma chini ya ufadhili wa Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi inayoratibiwa na Ofisi hiyo wakati alipofuatilia utekelezaji wake
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akifuatilia shughuli za mafunzo ya ufundi stadi anayopata Mwanafunzi Halima Shaibu wa fani ya Ufundi Bomba wa Chuo cha Ufundi Stadi  Don Bosco Dodoma anaye fadhiliwa na Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi inayoratibiwa na ofisi hiyo wakati alipofuatilia utekelezaji wake
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof..Joyce Ndalichako akifuatilia shughuli za mafunzo ya fani ya Uashi kwa wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi Don Bosco Dodoma wanaofadhiliwa na Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi inayoratibiwa na ofisi hiyo, wakati alipofuatilia utekelezaji wake
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akisitiza jambo kwa wanafunzi wa Chuo cha VETA Dodoma wakati wa kufuatili autekelzaji wa Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi inayoratibiwa na ofisi hiyo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof..Joyce Ndalichako akikagua matango katika Kitalu nyumba yaliyolimwa na wanafunzi wa  chuo cha Don Bosco Dodoma kupitia Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi inayoratibiwa na ofisi hiyo wakati alipofuatilia utekelezaji wake tarehe 19 Julai 2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.