Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amezindua Muongozi wa Mafunzo ya Sayansi kwa Skuli za Sekondari Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiangalia Ngoma ya Msewe katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja. alipowasili katika viwanja vya Hoteli hiyo,kwa ajili ya Uzinduzi wa Muongozo wa Mafunzo ya Sayansi kwa Walimu wa Skuli za Sekondari Zanzibar, na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Mustafa Kitwana na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na (kulia kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohammed Mussa
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiangalia Ngoma ya Msewe katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja. alipowasili katika viwanja vya Hoteli hiyo,kwa ajili ya Uzinduzi wa Muongozo wa Mafunzo ya Sayansi kwa Walimu wa Skuli za Sekondari Zanzibar, na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Mustafa Kitwana na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na (kulia kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohammed Mussa
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Meneja Mwandamizi wa Good Neighbors Tanzania John Messenza akitowa maelezo ya Vitabu vya muongozo wa Elimu ya Sayansi,Hesabati na Kingereza  wakati akitembelea maonesho hayo ya nyenzo za kufundishia masomo ya Sayansi, Hesabati na Kingereza katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja Wilaya ya Magharibi “B” Unguja na (kulia kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohammed Mussa na (kushoto kwa Rais) Balozi wa Korea ya Kusini Nchini Tanzania Mhe.Sun Pyo Kim na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali Abdulgulam Hussein.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, wakati ukipigwa wimbo wa Taifa wa Zanzibar, Tanzania na wa Afrika Mashariki, kabla ya kuaza kwa Uzinduzi wa Muongozo wa Mafunzo ya Elimu ya Sanyasi Zanzibar, na (kulia kwa Rais) Balozi wa Korea ya Kusini Nchini Tanzania Mhe. Sun Pyo Kim,Mkurugenzi Mkaazi wa KOICA Tanzania Bw. Kyucheol Eo na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohammed Mussa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Mustafa Kitwana.
Mkurugenzi Mkaazi wa KOICA Tanzania Bw.Kyucheol Eo akizungumza na kutowa maelezo ya mpango wa utekelezaji wa Mafunzo ya Sayansi kwa Walimu wa Skuli za Sekondari Zanzibar, wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Muongozo wa Mafunzo ya Sayansi, Hesabati na Kingereza Zanzibar, uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi "B"Unguja leo 3-8-2022. 
Mkurugenzi Mkaazi wa  Good Neighbors Tanzania Bi.Soni Juno akizungumza na kutowa maelezo ya mpango wa utekelezaji wa Mafunzo ya Sayansi kwa Walimu wa Skuli za Sekondari Zanzibar, wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Muongozo wa Mafunzo ya Sayansi, Hesabati na Kingereza Zanzibar, uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi "B"Unguja leo 3-8-2022. 
Balozi wa Jamhuri ya Korea ya Kusini Nchini Tanzania Mhe. Sun PyoKim akizungumza na kutowa salamu ya Nchi yake wakati wa Uzinduzi wa Muongozo wa Mafunzo ya Sayansi,Hesabati na Kiingereza kwa Walimu wa Skuli za Sekondari Zanzibar, wakati wa hafla ya Uzinduzi  huo uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi "B"Unguja leo 3-8-2022. RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika hafla ya Uzinduzi wa Muongozo wa Mafunzo ya Sayansi, Hesabati  na Kingereza kwa Skuli za Sekondari Zanzibar, uzinduzi huo uliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 3-8-2022.
BAADHI ya Watendaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akihutubia na kuzindua Muongozo wa Mafunzo ya Sayansi kwa Skuli za Sekondari Zanzibar, uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 3-8-2022.
WAGENI Waalikwa katika hafla ya Uzinduzi wa Muongozo wa Mafunzo ya Elimu ya Sayansi kwa Skuli za Sekondari Zanzibar, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akihutubia na kizindua Muongozo huo, uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja  leo 3-8-2022.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Vitabu vya Muongozo wa Mafunzo ya Sayansi,  Hesabati na Kingereza na Balozi wa Korea ya Kusini Nchini Tanzania Mhe. Sun Pyo Kim (kulia kwa Rais) na Mkurugenzi Mkaazi wa KOICA Tanzania Bw.Kyucheol Eo na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohammed Mussa, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Mustafa Kitwana  na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali Abdulgulam Hussein.

(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.