Habari za Punde

Waziri Mhe Jafo Amekutana na Kuzungumza na Balozi wa Misri Nchini Tanzania

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na Balozi wa Misri nchini Tanzania Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa alipofika Ofisi ya Makamu wa Rais Dar es Salaam leo Agosti 18, 2022 katika kikao kilichozungumzuia masuala mbalimbali yakiwemo maandalizi ya Mkutano wa 27 wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianch unaotarajiwa kufanyika nchini Misri Novemba mwaka huu. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na Balozi wa Misri nchini Tanzania Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa alipofika Ofisi ya Makamu wa Rais Dar es Salaam kufanya mazungumzo leo Agosti 18, 2022 kuzungumzuia masuala mbalimbali yakiwemo maandalizi ya Mkutano wa 27 wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi unaotarajiwa kufanyika nchini Misri Novemba mwaka huu. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mazingira Dkt. Andrew Komba.

Balozi wa Misri nchini Tanzania Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa akimkabidhi zawadi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo mara baada ya kufanya mazungumzo katika Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam leo Agosti 18, 2022 kuhusu maandalizi ya Mkutano wa 27 wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi unaotarajiwa kufanyika nchini Misri Novemba mwaka huu. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Misri nchini Tanzania Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa mara baada ya kumalizi kikao ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Agosti 18, 2022 kuzungumzuia masuala mbalimbali yakiwemo maandalizi ya Mkutano wa 27 wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi unaotarajiwa kufanyika nchini Misri Novemba mwaka huu.

(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Misri nchini Tanzania Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa katika Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam leo Agosti 18, 2022.

Pamoja na mambo mbalimbali kikao hicho kimezungumzuia maandalizi ya Mkutano wa 27 wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP27) unaotarajiwa kufanyika nchini Misri Novemba mwaka huu.

Dkt. Jafo alisema hii ni heshima kubwa kwa Bara la Afrika kushiriki katika mkutano huo na kwamba ushiriki wa Tanzania utatoa fursa katika kutangaza namna inavyoshirikiana na wadau katika hifadhi ya mazingira.

“Nikiri wazi ushiriki wetu kule Misri utakuwa mzuri na mpana na tayari tumeanza kufanya maandalizi ya ushiriki tukiwa taasisi zetu na wadau wegine ambapo tunatarajia kuonesha kazi zetu kupitia mkutano huo," alisema.

Aliongeza kuwa Tanzania itaendelea kusukuma ajenda ya kuzitaka nchi nchi zinazoendelea kutoa fedha barani Afrija kwa ajili ya kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kwa upande wake Balozi Mhe. Abulwafa alisema nchi yake inatarajia Tanzania itanufaika na COP27 kwa vile ni mojawapo ya nchi zinazoathiriwa na mabadiliko ya tabianchi.

Hata hivyo, alipongeza jitihada zinazofanywa na Tanzania katika kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.