Habari za Punde

RC Mhe. Mgumba Amewataka Wahitimu wa Mafunzo ya Operesheni Mabeyo 2022 Kutumia Mitandao ya Kijamii kwa Tija

MKUU wa Mkoa wa Tanga Mhe.Omari Mgumba kulia  akikagua gwaride maalum la Vijana wahitimu mafunzo kwa mujibu wa Sheria Operesheni Jenerali Venance Mabeyo Kikosi cha 835 KJ cha Mgambo JKT Wilayani  Handeni  Mkoani Tanga
Gwaride la vijana wahitimu wa mafunzo kwa mujibu wa sheria Operesheni Jenerali Venance Mabeyo kikosi cha 835 KJ cha Mgambo JKT wilayani  Handeni  Mkoani Tanga wakipita mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo
Gwaride la vijana wahitimu wa mafunzo kwa mujibu wa sheria Operesheni Jenerali Venance Mabeyo kikosi cha 835 KJ cha Mgambo JKT wilayani  Handeni  Mkoani Tanga wakipita mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo

Na Oscar Assenga HANDENI.

MKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba amewataka vijana waliohitimu wa mafunzo ya Operesheni Mabeyo 2022 wanakwenda kujiunga na vyuo vikuu hapa nchini kuhakikisha wanatumia vizuri mitandao ya kijamii kwa faida ikiwemo kujiepusha  na matumizi mabaya.na sio vyenginevyo

RC Mgumba aliyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya katika kambi ya JKT Kabuku 835 KJ wilayani Handeni wa mujibu wa Sheria Operesheni Jenerali Venance Mabeyo 2022,ambapo alisema kwa sababu vijana wengine waliopo vyuoni wamekuwa na uhuru uliopitiliza na kufanya mambo bila uwepo wa usimamizi.

Alisema lazima wazazi washirikiane katika kuwatembelea watoto wao mara kwa mara kwa maana unaweza kujua mtoto wao anasoma kumbe anasomeshwa jambo ambalo baadae linaweza kuwa na athari kwake na Jamii kwa ujumla.

"Niwasihi wazazi wenzangu muwe mnafanya kuwatembelea watoto wenu wanapokuwa vyuoni lakini wahitumu leo niwaase mkatumie vizuri mitandao ya kijamii kwa ajili ya faida na sio nyenginevyo maana vijana wengine waliopo vyuoni anaweza kudanganywa mwenye mitandao ya kijamii ukashurutishwa jambo ambalo unaweza kufanya kwa tamaa"Alisema

Mkuu huyo wa Mkoa alisema matokeo yake wanadhalilisha wazee wao Jamii na Ndugu na Taifa kwa ujumla hivyo hakikisheni suala la nidhamu wanalishikilia kweli hasa wale wanaoenda kuishi vyuoni.

"Kwa sababu mtakumbana na watu mbalimbali ikiwemo wanasheria wasije kuwapotosha nyie mmeiva na mmefundwa nidhami na uadilifu kaishini maisha hayo"Alisema Mkuu huyo wa Mkoa.

Awali akizungumza wakati wa ufunguji wa mafunzo hayo Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) Meja Jenerali Rajab Mabele aliwataka wahitimu wa mafunzo wasiende kutu mika vibaya katika maeneo mrakayokuwepo wakati wote mkumbuke kiapo mlichoapa.

Alisema kuwa kama wanavyofahamu majukumu ya JKT ni malezi ya vijana na uzalishaji wa mali na kufanya shughuli za ulinzi wa Taifa katika kutekeleza majukumu hayo ya kila siku.

Hata hivyo alisema hivyo kutolewa mafunzo hayo kwa vijana wa mujibu wa sheria na mafunzo ya mujibu wa sheria op Jenarali Mabeyo yamekuchukua muda wa majuma 12 mfululizo.

Mkuu wa JKT alisema kwamba wahitimu hao wamejifunzamasomo mbalimbi yakiwemo ya uzalishaji mali,nadharia na vitendo kwa ujumla lengo kukuza moyo wa uzalendo kuwajengea nidhamu ,ukakamavu na ujasiri.

Alisema hiyo itawafanya wajitambue kuwa ni sehemu ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuilinda,kuijenga na kuitetea nchi yao.

Naye kwa upande wake Mkuu wa Kikosi cha 835 KJ JKT Kabuku Luteni Kanali Raymond Mwanri alisema vijana hao wakiwa kwenye mafunzo hayo wamejifunza mambo mbalimbali ikiwemo ulinzi wa Taifa lao,Uzalendo na utii kwa mamlaka zilizowekwa kwa mujibu wa sheria .

Hata hivyo aliwataka wahitimu hao kuhakikisha wanakiishi kiapo hicho huku akieleza wamefaulu katika viwango mbalimbali vya kuhitimua mafunzo hayo.

Hata hivyo kwa upande Mkuu wa Mafunzo wa JKT Tanzania Kanali Aisha Matanza alisema mafunzo ya vijana ya kujitolea kwa mujibu wa sheria ya Jenero Mabeyo yamekuwa chachu kuweza kuwaimarisha vijana kuwafanya wakakamavu na wazalendo kwa nchi yao.

1 comment:

  1. Naitwa iddy Adam sunga nimehitim kidato cha nne mwaka 2022 .Naomba nafasi ya jkt .nahaidi kua mtihifu na muaminifu na kulitumikia taifa letu. asante. Natumaini nitafanikiwa.inshallah

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.