Habari za Punde

Rais Dk.Hussein Ali Mwinyi afungua Mkutano wa mwaka wa Jumuiya ya Kimataifa ya Wachakata Nafaka,

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kuufungua Mkutano wa mwaka wa Jumuiya ya Kimataifa ya Wachakata Nafaka,uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Unguja Jijini Zanzibar leo 26-10-2022 na kuwashirikisha Wadau wa viwanda kutoka Nchini mbalimbali.(Picha na Ikulu)
WASHIRIKI wa Mkutano wa Mwaka wa Jumuiya ya Kimataifa ya Wachakata Nafaka, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kuufungua mkutano huo unaofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Unguja Jijini Zanzibar leo 26-10-2022.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi maalum iliyotolewa na Jumuiya ya Kimataifa ya Wachakata Nafaka na Bw. Mounir Bakhressa na  (kulia kwa Rais) Mkurugenzi wa Kanda wa Jumuiya hiyo Bw.Ali Habaj, baada ya kuufungua mkutano wa Jumuiya ya Kimataifa ya Wachakata Nafaka, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Unguja Jijini Zanzibar leo 26-10-2022.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Buhler Bw.Matthias Grabe, wakati akitembelea maonesho ya Wafanyabiashara ya  Jumuiya ya Kimataifa ya Wachakata Nafaka, baada ya kuufungua mkutano wa mwaka wa jumuiya hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Unguja Jijini Zanzibar leo 26-10-2022 na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe.Omar Said Shaban.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Afisa Masoko wa Kampuni ya Viterra Bw.Joast Viehoff, wakati akitembelea maonesho ya Wafanyabiashara ya  Jumuiya ya Kimataifa ya Wachakata Nafaka, baada ya kuufungua mkutano wa mwaka wa jumuiya hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Unguja Jijini Zanzibar leo 26-10-2022 na (kulia kwa Rais) Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe.Omar Said Shaban na (Kushoto kwa Rais) Mkurugenzi wa Bakhressa Group Bw.Mounir Bakhressa.(Picha na Ikulu)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.