Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Lela Muhammed Mussa akiwasalimia Wanafunzi wakati wa ziara yake kutembelea Skuli za Mkoa wa Kaskazini Unguja na kuzungumza na Wanafunzi waliuorejea Skuli na Wanaojiandaa na Mitihani ya Darasa la Nne na la Saba.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Lela Muhamed Mussa amefanya ziara ya kutembelea Wanafunzi ambao wamerejea skuli baaada ya kuacha masomo kutokana na sababu mbalimbali za kimaisha na kifamilia katika Mkoa wa kaskazini Unguja.
Katika ziara hiyo Waziri Mhe.lela alipata fursa ya kukagua ujenzi wa madarasa ya Elimu mbadala pamoja na kuzungumza na wanafunzi ambao wanajitarisha kufanya mitihani ya Taifa ya darasa la nne na saba katika skuli ya Bububu ambapo aliwata kusoma kwa bidii ili kuweza kujitarisha na mitihani yao ambayo inatarajiaa kuanza mapema wiki ijayo.
Aidha amewataka Walimu Wakuu kuwasimamia pamoja na wasimamizi wa mitihani kuwa waadilifu na kujiepusha na vindendo vyovyote ambayo vitapelekea kuleta taharuki wakati zoezi la ufanyaji mitihani likiendelea.
No comments:
Post a Comment