Habari za Punde

Kundi la Watoto na Vijana Wahanga Zaidi ya Masuala ya Usalama Barabarani Nchini

 

MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandiliwa akizindua wa mpango kazi wa safari Salama na Endelevu kwa ajili ya Jiji la Tanga kwa shule za Msingi na Sekondari unaotekelezwa na Shirika hilo kupitia ufadhili wa Botnar Foundation na Jiji la Tanga wakiwemo wadau wengine. kushoto ni Meneja Mkazi wa Shirika la Amend Tanzania Saimoni Kalolo 

MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandiliwa akizindua wa mpango kazi wa safari Salama na Endelevu kwa ajili ya Jiji la Tanga kwa shule za Msingi na Sekondari unaotekelezwa na Shirika hilo kupitia ufadhili wa Botnar Foundation na Jiji la Tanga wakiwemo wadau wengine. kushoto ni Meneja Mkazi wa Shirika la Amend Tanzania Saimoni Kalolo 
MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandiliwa akizindua wa mpango kazi wa safari Salama na Endelevu kwa ajili ya Jiji la Tanga kwa shule za Msingi na Sekondari unaotekelezwa na Shirika hilo kupitia ufadhili wa Botnar Foundation na Jiji la Tanga wakiwemo wadau wengine. kushoto ni Meneja Mkazi wa Shirika la Amend Tanzania Saimoni Kalolo 

Meneja Mkazi wa Shirika la Amend Tanzania Saimoni Kalolo  akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango kazi wa safari Salama na Endelevu kwa ajili ya Jiji la Tanga kwa shule za Msingi na Sekondari unaotekelezwa na Shirika hilo kupitia ufadhili wa Botnar Foundation na Jiji la Tanga wakiwemo wadau wengine. 
MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo
MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo

Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhman Shilloo akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo

Mwakilishi wa Mkuu wa Usalama barabarani Mkoa wa Tanga  George Elihaki  akieleza mipango yao


Mwakilishi wa Wakala a Barabara nchini (Tanroad) kitengo cha Usalama barabarani Felician Lwiza 




Na Oscar Assenga,TANGA.

KUNDI la Watoto na Vijana kati ya miaka 5 mpaka 29 ndio waathirika zaidi ya masuala ya usalama barabarani katika Bara la Afrika, Tanzania na Ulimwenguni kote imeelezwa kwa hiyo ni eneo ambalo linahitaji jitihada kubwa maana wapo barabarani siku zote wakitafuta maisha .

Hayo yalielezwa na Meneja Mkazi wa Shirika la Amend Tanzania Saimoni Kalolo wakati uzinduzi wa mpango kazi wa safari Salama na Endelevu kwa ajili ya Jiji la Tanga kwa shule za Msingi na Sekondari unaotekelezwa na Shirika hilo kupitia ufadhili wa Botnar Foundation na Jiji la Tanga wakiwemo wadau wengine.

Katika mradi huo unawalenga hasa walengwao wao wakubwa wanafunzi,kundi la watoto na vijana ambao wamekuwa wakifanya shughuli za kila siku na hawachukui tahadhari na kundi ambalo lipo kwenye hatari kubwa za usalama barabarani ambapo kitakwimu Afrika kusini mwa jangwa la Sahara ajali zimekuwa ni nyingi sana.

“Kitakwimu Afria Kusini Mwa Jangwa la Sahara ajali zimekuwa nyingi lakini cha kushangaza bara hilo lina magari machache kuliko yote jambo ambalo tunahitaji nguvu ya pamoja kuhakikisha tunaliondoka tatizo hilo “Alisema

Hata hivyo alisema kikubwa zaidi wanapoteza zaidi ya asilimia 3 ya Pato la Taifa kutokana na ajali za barabarani hibyo lazima jithaza ziweze kuchukuliwa kwa kasi zaidi.

Awali akizungumza wakati akizundua mpango huo,Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa ameitaka Jamii ione umuhimu wa kulinda miundondu iliyopo barabarani.

Alisem kutokana na kwamba kwenye kila miradi inayofanywa na serikali inakwenda sambamba na uwekaji alama za usalama za barabarani na wakati mwengine wanaweka mpaka kamera na kumekuwa kunaripotiwa na baadhi ya matukio watu kuanza kupita na kuiba baadhi ya vitu.

Alisema kwa Tanga kulikuwa na mradi wa kufunga Taa lakini baadhi ya watu wanalikuwa wanapita na kuiba hivyo alitumia hadhara hiyo kuwaomba wajumbe na jamii kuona umuhimu wa kulinda hizo rasilimali wanazokuwa nazo na miundombinu wakifanya hivyo wanaweza kuokoa maisha ya watu na watu ambao wanaweza kupata ulemavu kutokana na changamoto za utoaji wa alama hiuzo za bareabarani.

“Nisisitize wajibu wa Amend kuendelea kutoa elimu ya usalama barabarani kwani Tanzania kuna kundi kubwa la vijana wamejiajiri kupitia bodaboda aina ya vijana wanaofanya shughuli hizo wakati mwengine imekuwa ni mtihani wanapofundishwa huwa wanarudia mara kwa mara hivyo waendelee kutoa elimu”Alisema Mkuu huyo wa wilaya.

“Kwanza kwa wale ambao hawana taaluma ya udereva kuna wale ambao wana elimu na leseni wakati mwengine wanajisahau kufanya maamuzi ya hovyo wao waendelee kuwakumbusha vi vema wakaendelea kutiii sheria za usalama barabarani”Alisema.

Awali akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo Kaimu Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Tanga George Elihaki alisema kwa kushiikiana na Taaasisi ya Amend wameweza kutoa elimu ya usalama barabarabi kwa bodaboda 500.

Alisema kwamba elimu hiyo imesaidia kuweza kuwabadilisha tabiaa baada ya waendesha pikipiki hao huku akieleza kitendo cha kuja na mradi ambao unagusa masuala la usalama barabarani wanaona watakwenda kupunguza kwa kiwango kikubwa ajali ambazo zingepoteza nguvu kazi ya Taifa.

“Lakini zingepoteza watu aamabao kesho na kesho wangekuwa regemezi hivyo nieapongeza kwa ubunifu mzuri kwa, mradi huoi ambao wanakawenda kuufanya wa

Hata hivyo kwa upande wake Mwakilishi wa Wakala a Barabara nchini (Tanroad) kitengo cha Usalama barabarani Felician Lwiza alisema wanafanya kazi ya kupanga mipango kwa ajili ya ujenzi wa barabarta na kujenga na kutunza.

Alisema katika kupanga wanahakikisha barabara zinapita kwenye maeneo salama na kuzingtia himilifu kwa bajeti kukarabaratika kujenga wanahakikisha barabara zinazingatia uwezo wa barabara maana uzito wa magari na miteremko na miinuko inakuwa katika hali ya salama.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.