Habari za Punde

Rais Mstaafu Jaklaya Kikwete ziarani Zanzibar

Rais Mstaafu Awamu ya Nne Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri wa Afya Nassor Ahmed Mazrui mara baada ya kuwasili katika Kliniki ya Mama Wajawazito na Watoto pamoja na kuzalisha Sebleni kwa Wazee Zanzibar ikiwa ni ziara ya kuangalia utekelezaji wa Maazimio ya Mkutano wa 2019 wa UNFPA uliofanyika Nairobi kuhakikisha hakuna Vifo vya mama wajawazito na Watoto.
Rais Mstaafu Awamu ya Nne Jakaya Kikwete akizungumza na Madaktari Wauguzi na Wakunga  baada ya kuwasili katika Kliniki ya Mama Wajawazito na Watoto pamoja na kuzalisha Sebleni kwa Wazee Zanzibar ikiwa ni ziara ya kuangalia utekelezaji wa Maazimio ya Mkutano wa 2019 wa UNFPA uliofanyika Nairobi kuhakikisha hakuna Vifo vya mama wajawazito na Watoto
Waziri wa Afya Nassor Ahmed Mazrui akisalimiana na Mrithi wa Mfalme wa Denmak Mary Elizabeth mara baada ya kuwasili katika Kliniki ya Mama Wajawazito na Watoto pamoja na kuzalisha Sebleni kwa Wazee Zanzibar ikiwa ni ziara ya kuangalia utekelezaji wa Maazimio ya Mkutano wa 2019 wa UNFPA uliofanyika Nairobi kuhakikisha hakuna Vifo vya mama wajawazito na Watoto.
Daktari Mkuu wa Kliniki ya Mama Wajawazito na Watoto pamoja na kuzalisha Sebleni kwa Wazee Zanzibar Abdulkadir Abdalla Idarous akitoa maelezo kwa Mrithi wa Mfalme wa Denmak Mary Elizabeth wakati akitembelea  Kliniki ya Mama Wajawazito na Watot ikiwa ni ziara ya kuangalia utekelezaji  wa Maazimio ya Mkutano wa 2019 wa UNFPA uliofanyika Nairobi kuhakikisha hakuna Vifo vya mama wajawazito na Watoto.
Rais Mstaafu Awamu ya Nne Jakaya Kikwete akiwa pamoja na Mrithi wa Mfalme wa Denmak Mery Elizabeth wakipatiwa maelezo na Daktari Mkuu wa Kliniki ya Mama Wajawazito na Watoto pamoja na kuzalisha Sebleni kwa Wazee Zanzibar Abdulkadir Abdalla Idarous  kuhusu huduma  zinazotolewa na Chanjo kwa wazazi wakati wakitembelea baadhi ya Vymba katika Kliniki hio. ikiwa ni ziara ya kuangalia utekelezaji  wa Maazimio ya Mkutano wa 2019 wa UNFPA uliofanyika Nairobi kuhakikisha hakuna Vifo vya mama wajawazito na Watoto.

.
Rais Mstaafu Awamu ya Nne Jakaya Kikwete akionesha kitu wakati wakitembelea Kliniki ya Mama Wajawazito na Watoto Sebleni Zanzibar  ikiwa ni ziara ya kuangalia utekelezaji  wa Maazimio ya Mkutano wa 2019 wa UNFPA  uliofanyika Nairobi kuhakikisha hakuna Vifo vya mama wajawazito na Watoto
Waziri wa Afya Nassor Ahmed Mazrui akitoa hotuba  kwa Viongozi na wananchi waliohudhuria  Kliniki ya Mama Wajawazito na Watoto pamoja na kuzalisha Sebleni kwa Wazee Zanzibar ikiwa ni ziara ya kuangalia utekelezaji wa Maazimio ya Mkutano wa 2019 wa UNFPA uliofanyika Nairobi kuhakikisha hakuna Vifo vya mama wajawazito na Watoto.
Waziri wa Afya Nassor Ahmed Mazrui akimkabidhi Zawadi ya Mlango Mrithi wa Mfalme wa Denmak Mary Elizabeth mara baada ya kumaliza kutembelea  sehemu mbalimbali za Klinik ya ama Wajawazito na Watoto pamoja na kuzalisha Sebleni kwa Wazee Zanzibar ikiwa ni ziara ya kuangalia utekelezaji wa Maazimio ya Mkutano wa 2019 wa UNFPA uliofanyika Nairobi kuhakikisha hakuna Vifo vya mama wajawazito na Watoto.

Rais Mstaafu Awamu ya Nne Jakaya Kikwete ambae pia ni Mwenyekiti Mwenza wa UNFPA akitoa hotuba baada ya kumaliza kutembelea  sehemu mbalimbali za Klinik ya mama Wajawazito na Watoto pamoja na kuzalisha Sebleni kwa Wazee Zanzibar ikiwa ni ziara ya kuangalia utekelezaji wa Maazimio ya Mkutano wa 2019 wa UNFPA uliofanyika Nairobi kuhakikisha hakuna Vifo vya mama wajawazito na Watoto.


PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Na Rahima Mohamed            Maelezo          9/11/2022

 

RAIS Mstahafu wa awamu ya tano wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amesema Shirika la Maendeleo linaloshuhuikia idadi ya watu na Maendeleo Dunuani (UNFPA) limejipanga kuhakikisha kwamba vifo vya mama na mtoto vinavyotokana na uzazi vinapungua duniani.

 

Akizungumza mara baada ya kukagua huduma za afya zinatolewa katika kituo cha afya Amani Kwa Wazee Mkoa wa Mjini Mgharibi Unguja,Dk. Kikwete amesema mkakati huo ni kuhakikisha madaktari wanaendelea kutoa huduma bora ambapo Shirika hilo litaendelea kutoa vifaa tiba na kupunguza kesi za vifo vya watoto wachanga.

 

Rais huyo ambae pia ni Mwenyekiti wa Shirika hilo kwenye masuala ya afya amesema Shirika hilo limefanya mkutano juu ya mkakati wa kutoa huduma bora za afya nchini Cairo mwaka 1994 na azimio la mkutano huo umefanyika Nairobi mwaka 2019 ili kuona linaendelea kusimamia upatikanaji wa huduma bora za afya.

 

Aidha Rais Kiwketwe amekipongeza kituo hicho kwa kudhibiti vifo vya mama na mtoto kuhakikisha kipindi cha Januari hadi sasa   hakijatokea kifo chochote.

 

Waziri wa afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui, amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaendelea na mkakati wa kupunguza vifo vya mama na mtoto katika vituo na hospitali Unguja na Pemba sambamba kuongeza vifaa vya tiba na wataalamu wa afya.

 

meisema Serikali kupitia fedha za Uviko 19 itajenga Hospitali nyengine 11 lengo kupunguza matatizo ya vifo kwa akinamama na kuongeza huduma bora za matibabu kwa wananchi.

 

Amelishukuru Shirika hilo kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuongeza huduma za matibabu na kumtaka Rais huyo kuendelea kuunga mkono utoaji wa huduma hizo za afya.

 

Mkurugenzi Kinga kutoka Wizara ya Afya Zanzibar Dk. Salim Slim amesema Kituo cha afya cha Amani Kwawazee kinakabiliwa na upungufu wa vifaa tiba ikiwemo vifaa vya kupimia maradhi mbalimbali na kusababisha usumbufu kwa wagonjwa.

 

Ameeleza kuwa kukosekana kwa elimu ya afya ya uzazi kwa mama wajawazito kunachangia akinamama kutokubali kutumia huduma ya uzazi wa mpango.

 

 Katika Ziara hiyo Dk. Kikwete alifuatana na mtoto wa malkia wa Denmark HRH. Croun Princes Mary na kutembelea kituo cha afya Kwawazee pamoja na kusikiliza changamoto zilizopo.

 

Aidha RAIS Jakaya Mrisho Kikwete kesho anatarajiwa kuwa mwenyeji wa Uzinduzi wa ripoti ya ufuatiliaji wa mkutano wa idadi ya watu na maendeleo itakayofanyika Hoteli ya Melia.

 

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.