Habari za Punde

Aziz Ki Aing’arisha Yanga Ugenini Dhidi ya Mtibwa Sugar. Yafikisha Alama 50 Ligi Kuu ya NBC Yailaza Mtibwa Sugar 1-0

 
KIUNGO Mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki ameing’arisha timu yake ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar kwa kuifunga bao 1-0 mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa katika uwanja wa Manungu Turiani Mkoani Morogoro.

Yanga walipata bao kunako dakika ya 26 likifungwa na Stephane Aziz Ki  kwa faulo ya moja kwa moja iliyomshinda mlinda mlango wa Mtibwa Sugar baada ya Kibwana Shomari kuchezewa rafu.

Kwa ushindi huo Yanga  SC wamefikisha Pointi 50 na kuwaacha watani zao Simba SC kwa tofauti ya Pointi 7 ,Simba wakiwa nafasi ya pili wakiwa na Pointi 44.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara timu ya Yanga imeendelea kujishindilia kileleni mwa msimamo wa Ligi hiyo kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Katika mchezo huo uliopigwa leo Disemba 31,2022 kwenye uwanja wa  Manungu Turiani, Morogoro timu ya Yanga ilipata bao katika dakika ya 26 ya mchezo huo, goli likifungwa na Stephanie Azizi Ki kwa mpira wa adhabu uliomshinda mlinda mlango wa Mtibwa Sugar.

Katika kipindi cha pili cha mchezo huo timu zote zilionekana kushambuliana ambapo katika dakika ya 77 ya mchezo huo timu zote zilifanya mabadiliko huku Yanga ikiingiza wachezaji watatu  na Kagera Sugar ikiwaingiza washambuliaji wawili Onesmo Mayaya na Joseph Mkele.

Hata hivyo mabadiliko hayo hayakuweza kuzaa matunda kwa timu ya Mtibwa Sugar na kufanya kutoka uwanjani wakiwa wamekubali kichapo cha bao 1-0.

Kufuatia ushindi huo timu ya Yanga imeendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa Ligi ya NBC Tanzania Bara kwa kuwa na alama 50 wakizidi kumuacha mpinzani wake wa karibu Simba SC yenye alama 44.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.