RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka wadau kwenye
sekta ya utalii kuboresha huduma ziendane na mazingira ya wakati uliopo ili kukidhi
haja na mahitaji ya wageni wanaoitembelea Tanzania.
Dk. Mwinyi alieleza
hayo alipofungua tamasha la utalii na biashara “The Z- Summit” huko ukumbi
wa Golden Tulip, Uwanja wa Ndege wilaya ya mjini.
Alisema sekta ya
utalii Zanzibar nyenye vivuti vingi ni sekta muhimu inayochangia asilimia 30 ya
pato la taifa.
Dk. Mwinyi alisema
Serikali ya Mapinduzi ya Zanazibar imechukua jitihada mbalimbali kuimarisha
sekta hiyo yenye lengo la kuongeza watalii kufikia 850, 000 ifikapo mwaka 2025
ambapo tayari imeimarisha miundombinu ikiwepo kutanua barabara za kisasa,
kuboresha uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume ambapo alieleza
kwa sasa unatoa huduma za kimataifa zenye kukidhi haja ya mahitaji ya wageni
chini ya uongozi wa taasisi ya kimaifaifa ya DNATA inayotoa huduma za kimataifa
za viwanja vya ndege.
Alisema ujenzi wa
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Pemba unaotarajiwa kuifungua Pemba kiutalii ni
miongoni mwa juhudi za sreikali kwenye kukuza sekta ya utalii nchini.
Alisema Zanzibar ni
kituo cha wageni wengi kutoka mataifa mbalimbali ya dunia kilivyopambwa na
magofu yaliyohifadhi historia pamoja na mji mkongwe uliokwenye hifadhi ya
UNESCO inawavutia wageni wengi kupitia fukwe angafu, ubuluu wa bahari pamoja na
ukijani wa visiwa vyake vilinavyopambwa na michezo ya baharini
Alieleza milango ya
serikali ikowazi kuwakaribisha wawekezaji kuekeza kwenye michezo ya baharini
ikiwemo gamu za baharini na michezo ya fukwe za bahari ikiewemo volleyball.
Akizungumzia Sera ya
uchumi wa bluu na utalii Dk. Mwinyi alieleza Serikali imechukua jitihada kubwa
kuitekeleza sera hiyo kwa vitendo iliwa pamoja na kutilia mkaazo suala la
endelevu kupitia sera yake ya “utalii kwa wote”.
Aliahidi kuwa
serikali itaendelea kuwawekeza mazingira mazuri wadau wote wa utalii na
kuwaomba mkutano huo uwe chachu ya kutoa firsa nyingi kwa watalii na wadau
wake. Hivyo alisema ni imani kwamba mkusanyiko huo ulioshirikisha wadau
mbalimbali wa sekta utatoa mafanikio mazuri katika kuikuza sekta nchini.
“Sote kwapamoja
tuungane kubadilishana uzoefu, kufanyakazi pamoja tutachangia kuikuza sekta ya
utalii, Tanzania
Akizungumzia suala la
kutunza mazingira endelevu, Rais Dk. Mwinyi alisema utalii ni chachu ya
uchafuzi wa mazingira, hivyo aliitaka jamii, wadau wa utalii pamoja na
wawekezaji kwenye sekta hiyo, kutunza mazingira na viumbe vya bahari, kuepuka
ujaribifu wa ikolojia, uharibifu wa ardhi, uchafuzi wa hew na maji kwa kuweka
mazingira na utalii endelevu.
Mapema Waziri wa
Utalii na Maliasili wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Muhamed Omary Mchengerwa
alieleza hali ya utalii ilivyo duniani, Tanzania inakazi kubwa ya kuitangaza
nchini kimataifa kupitia sekta ya utalii.
Alisema kwa Serikali
ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa usjirikiano wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar wanalengo la kuongeza watalii wengi kutoka mataifa makubwa duniani ikiwemo
bara Ulaya, Asia, Mashariki ya Mbali na Amerika
Aidha alieleza
serikali pia zina nia ya kuliteka soko la utalii kutoka China ambao wanaongoza
dunia kutoa watalii wengi hadi kufikia milioni moja na nusu kwa kila nchini.
Naye, Waziri wa
Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Simai Muhammed Said
alisema wakati umefika kwa Zanzibar kubadili mtazamo kupitia misimu ya utalii
kuondokana na dhana msimu mdogo na mkubwa badala yake wawetayari kuutangaza
utalii misimu yote iwanufaishe wao na taifa kwa ujumla.
Mwenyekiti wa ZATI
ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii, Rahim Baloo alisema mkutano huo
umelenga kuitambulisha dunia na kuitangaza Zanzibar kiutalii na kiutamaduni pamoja
na kuwa kuwakaribisha wawekezaji zaidi. Aidha, aliipomgeza serikali awamu na
nane na wizara kwa ujumla kwa kuziungamkono sekta binafsi mchango mkubwa
wanaoutoa kwa uchumi wa Zanzibar.
IDARA YA MAWASILIANO
– IKULU, ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment