MWENYEKITI wa Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akikabidhiwa Mikoba 100 ya Skuli na Balozi Mdogo wa China anayefanyia Kazi zake Zanzibar Mhe. Zhang Zhisheng ikiwa ni ahadi yake aliyoitowa wakati wa Maadhimisho ya mwaka mmoja wa Taasisi hiyo (ZMBF) hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za (ZMBF) migombani Wilaya ya Mjini Unguja leo 28-3-2023
Mama Mariam ameyasema
hayo ofisini kwake Migombani, Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mijini Magharibi, wakati akipokea
zawadi ya mikoba 100 ya skuli kutoka kwa Balozi Mdogo wa China aliepo Zanzibar,
Zhang Zhisheng ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake
aliyoitoa Machi 20, mwaka huu katika halfa ya kutimiza mwaka mmoja wa taasisi
ya “Zanzibar Maisha Bora Foundation” kwenye ukumbi wa Golden, Tulip, Uwanja wa
ndege, Zanzibar.
Alisema zawadi hizo
zimekuja muda sahihi kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambacho ni
kizuri kutoa na kuwapa wanaohitaji, hivyo aliahidi mikoba hiyo kuwapatia
wanafunzi wa skuli mbali mbali za Zanzibar.
Mama Mariam ambae pia
ni Mwanzilishi na Msarifu wa (ZMBF) alitumia fursa hiyo kuushukuru ubalozi
mdogo wa China kwa kutekeleza ahadi yao kivitendo kwa ZMBF pia kuendeleza ushirikiano
wa kirafiki uliopo kwa taasisi hiyo.
Alieleza Ubalozi
Mdogo wa China umeisaidia sana ZMBF hata kabla ya kukamilisha mwaka mmoja tokea
kuasisiwa kwake mwaka 2021 na kuzinduliwa mwaka 2022 na kueleza furaha yake
kuona ubalozi huo unafuatia kwa karibu harakati za maendeleo zinazofanywa na
ZMBF za kuisaidia jamii na Wazanzibar kwa ujumla.
Akizungumza kwenye
hafla hiyo, Balozi mdogo wa China, Zhang Zhisheng alisema anaamini zawadi hiyo
itawafaa na kufurahiwa na watoto wadogo wa shule.
Balozi Zhisheng alisema,
China na Zanzibar zimekua na ushirikiano wa kirafiki kwa muda mrefu na kwamba
uhusiano wao haukuishia tu kwa Serikali za Tanzania lakini kwa wa watu wa nchi
za pande mbili hizo ikiweo pia na taasisi binafsi zenye nia ya kuendeleza
malengo ya Serikali ikiwemo maendeleo kwa watu wao.
Alisema ubalozi mdogo
wa China kwa kushirikiana na Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation wamekua
wakifanyakazi bega kwa beka katika hatua za kuunga mkono maendeleo yanayofanywa
na Serikali ya Mapindizi ya Zanzibar kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Hata hivyo, ubalozi huo
umeahidi kuendelea kuiungamkono Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar hata asasi za
kiraia zinazoiungamkono serikali katika kuwaletea maendeleo watu wao.
Taasisi ya Zanzibar
Maisha Bora Foundation iliasisiwa tangu mwaka 2021 na kuzinduliwa mwaka 2022 ambapo
mwezi Februari mwaka huu ilitimiza mwaka mmoja tokea kuasisiwa na sasa
inatekeleza mpango mkakati wa miaka mitatu 2023 hadi 2025 ambao unatarajia
kutumia dola za Marekani milioni mbili ili kufanikisha malengo iliyojiwekea.
No comments:
Post a Comment