Habari za Punde

Mhe Othman ahimiza tuwe na utamaduni wa kupanda miti

 Mkoa wa Kusini Pemba

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Msoud Othman, amesema   athari zinazotokana na uharibifu wa mazingira Zanzibar ni kubwa na  kwamba ni lazima wananchi , viongozi na taasisi mbali mbali kuungana na kuwa na utamaduni wa kupanda miti na kuithamini ili kulikabili janga hilo. 

Mhe. Othman ameyasema hayo kwa nyakati tofauti katika mkutano  wake na Viongozi , masheha na wafanyakazi wa Mabaraza ya Mji wa Chake na Mkoani  Mkoa wa Kusini Pemba akiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo.

Mhe. Othman alikuwa akielekeza kuhusu na hali halisi ya uharibufu wa mazingira Zanzibar pamoja na haja ya viongozi na wananchi kushirikiana pamoja katika utekelezaji wa mpango wa Serikali wa wa urithi wa Kijani Zanibar unaotarajiwa kutekelezwa hivi karibuni  wenye lengo la kutunza, kulinda na kuhifadhi mazingira ya Zanzibar.  

Amewataka viongozi hao pamoja na wananchi kufahamu kwamba mpango huo unaotarajiwa kutekelezwa ni wa kitaifa ambao unatarajiwa kuisaidia sana Zanzibar kulinda na kuhifadhi mazingira yake ili kujikinga na majanga yatokanayo na athari za mabadiliko ya tabia nchi na binaadamu.

Mhe. Makamu amewaeleza viongozi hao na wananchi kuwa changamoto  iliyopo ya athari ya kimazinmgira Zanzibar inaendelea kuwa kubwa na iwapo hatua za pamoja hazitachukuliwa inaweza kuleata maafa ya ,kijamii na kiuchumi hapa Zanzibar.

Amesema kwamba hali ya uchafuzi na uharibifu wa mazingira tayari imechangia miti mingi ya asili ambayo ni ya matunda kuanza kupotea na kwamba kizazi kijacho hakitaweza kufaidika na rasilimazili zilizokuwepo ambazo wazazi wao wamechangia kuziharibu na kuzipoteza.

Aamesema mbali na uharibu huo wa mazingira pia  kasi ya ukaji wa watu halingani na hali uhifadhi wa mazingira ikiwemo kuchafuliwa na kupotea vyanzo  vya maji na hivyo wananchi kukosa huduma muhimu ya maji.

Amesema kwamba hivi sasa maeneo mengi ya Zanzinbar maji yameanza kupotea na kwamba visima vingi vya maji safi na salama vilazimika kuchimbwa kwa kina kirefu kwa kuwa maji yamepotea kutokana na kuharibika kwa mazingira.

Mhe. Othman amefahamisha kwamba hata eneo la kilimo a mbalo ni ukanda wa maghareibi ya visiwa vya unguja na pemba tayari limeatjhriwa na hali hiyo kwa kuendeleza shughuli za kibaadamu ukiwemo ujenzi wa nyumba za makaazi.

Amewataka viongozi wanaosimamia serikali za Mitaa kuhakikisha kwamba nazingatia na kusimamia ipasavyo sheria na taratibu za mipango miji ili Zanzibar isiendelee kuathariwa na matatizo ya kimazingira  na kuweza kuwarithisha vizazi vijavyo mazingira bora na salama.

Amewataka viongozi hao na wananchi kushirikiana na taasisi mbali mbali ili kuanza kujipanga kwa kuyain isha maeneo yanayohitaji kupandwa miti ya namna tofauti kulingana na uasili wa miti iliyokuwepo kwenye maeneo hayo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Matar Zahor Masoud amesema kwamba mbali na kuipokea  Mpango wa serikali kuu kuhusu kuirejesha Zanzibar kuwa ya kijani lakini katika ngazi za halimashauri na mikoa tayari wameandaa miakakatgi mbali mbali itayaoungana na mpango huo katika kulikabili suala la mazingira.

Amesema kwamba katika mpangowa wao wanakusudia kuwashirikisha na kuwarkithisha wanafunzi kutoka  ngazi za awali juu ya kupanda  na kuhifadhi miti katika maeneo ya skuli zao katika kipindi chote cha wanafunzi kuwepo kwao maskulini.

Nao wakurugenzi wa Mabaraza ya Miji ya Chake Ndugu Maulid  Mwalimu Ali na wa Mkoani Ndugu Yussuf Kaiza Makame wakiwasilisha ripoti ya utekelizaji wa shughuli za mabaraza hayo kwa kipindi cha nusu mwaka  wamesema kwamba shughuli nyingi licha ya kuwepo kwa changamoto mbali mbali, lakini wamefanikiwa kuzitekeleza kwa ufanisi mkubwa.

 

Mwisho

Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Kitengo chake cha habari leo tarehe 06/03/2023.    

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.