WASHIRIKI
wa Fainali ya Mashindano ya Kusoma Qur-an Tartiil, wakiwa katika ukumbi kabla
ya kuaza kwa mashindano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden
Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini
Zanzibar, yaliyodhaminiwa na Benki ya Watu wa Zanzibar.
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi
akimkabidhi ufungo wa Pikipiki (Bodaboda)mshindi wa Pili wa Fainali ya
Mashindano ya Kusoma Qur-an Tartiil Zanzibar. Mwanafunzi. Nassor Hamad Kombo,
baada ya kuibuka mshinda katika mashindano hayo ya fainali yaliyofanyika katika
ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi
“B” Unguja Jijini Zanzibar leo 19-4-2023
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi ufungo wa gari aina ya Toyota Alphard mshindi wa kwanza wa Fainali ya Mashindano ya Kusoma Qur-an Tartiil Zanzibar. Mwanafunzi. Said Ali Juma, baada ya kuibuka mshinda katika mashindano hayo ya fainali yaliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 19-4-2023. Na (kulia kwa Rais) Mkurugenzi Huduma za Kibenki PBZ Ndg. Said Mohammed Said
No comments:
Post a Comment