Habari za Punde

Huduma za Afya Zasogezwa Vijijini

 Afisa  mradi wa kuvifikia   vikundi vya wagonjwa wenye maradhi yasioambukiza kutoka PharmaAccess International Queen-Ruth Msina akimskiliza kwa makini mgonjwa wa maradhi hayo wakati alipokua akimpatia huduma za Afya huko Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja
Afisa  mradi wa kuvifikia   vikundi vya wagonjwa wenye maradhi yasioambukiza kutoka PharmaAccess International Queen-Ruth Msina akimskiliza kwa makini mgonjwa wa maradhi hayo wakati alipokua akimpatia huduma za Afya huko Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja
Afisa kutoka Wizara ya Afya kitengo cha Maradhi yasioambukiza Dkt Hafidh Abdul- Rahman Seif  alipokua akiwapatia elimu ya maradhi yasioambukiza wagonjwa wa maradhi hayo kabla ya kuanza kwa zoezi la utoaji wa huduma za Afya katika ngazi ya jamii lililoandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiiana na PharmAccess International huko Mahonda Mkoa wa  Kaskazini Unguja.

Na Fauzia Mussa    Maelezo Zanzibar

Kufuatia Wizara ya Afya kuamua  kusogeza huduma za afya  karibu na jamii kumepelekea kutatua changamoto  za  upatikanaji wa huduma hizo ambazo zilikua zikifuatwa masafa marefu.

Kauli hiyo imetolewa na Wazee wanaoishi na mardhi yasioambukiza wakati wakipatiwa huduma za afya ndani ya Jamiii huko Skuli ya Mkataleni Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja.

Walisemasema awali walikuwa wakifuata huduma hiyo masafa ya mbali jambo lililokuwa likiwapa usumbufu kutokana na hali zao.

"Licha ya kufuata huduma hizo mbali na maeneo yetu pia tunapofika vituoni tunakuta foleni kubwa  ya wagonjwa mbalimbali jambo ambalo linaturudisha nyuma kwenda klinik kila mwezi".walieleza wazee hao.

Walifahamisha kuwa   kuanzishwa kwa vikundi vya wagonjwa wenye maradhi yasioambukiza vijijini kunawapa Uhuru wa kujieleza kwani  Daktari hupata muda wa kutosha kumsikiliza na kumuhudumia mgonjwa ipasavyo

" kukutana  na madaktari kila mwezi maeneo kama haya nje ya spitali kunatuweka huru kwani tunapata elimu, tunabadilishana  mawazo na hata  uzowefu wa maradhi haya kwa vile  sote hapa ni wahanga wa maradhi yasioambukiza"

Aidha Wazee hao wanaoishi na maradhi yasioambukiza  Shehia ya Mkataleni wameishukuru Wizara ya Afya  na PharmAccess kwa kuwasogezea huduma za Afya karibu  na jamii.
Nae Afisa kutoka Wizara ya Afya kitengo cha Maradhi yasioambukiza Dkt. Hafidh Abdurahman Seif aliwashauri wazee hao kufuata masharti waliopangiwa na madaktari ikiwemo kuepuka vichocheo vinavyosababisha  maradhi hayo .
"Kuna  baadhi ya vichocheo   haviepukiki  kama urithi lakini vipo ambavyo  vinaepukika ikiwemo  utumiaji wa pombe ,tumbaku na sigara hivyo basi tujitahid kukaa navyo mbali"  alifahamisha Dkt. Hafidh .
 Dkt. Hafidh aliiomba  jamii kuachana na matumizi ya pombe ,tumbaku na uvutaji wa sigara uliopitiliza kwani unapelekea kupata   kisukari na saratani ya mapafu maradhi ambayo hayatibiki.
Alifahamisha kuwa Kwa siku binaadamu anatakiwa kutumia sukari  si zaidi ya kijiko kimoja hivyo aliitaka jamii kuachana na  matumizi ya sukari kupita kiasi.
Alisema ulaji usiozingatiwa mlo kamili  umekua ukichukua  asilimia kubwa  za ongezeko la maradhi yasioambukiza ikiwemo sindikizo la juu la damu.
" kiafya Kwa siku tunatakiwa kutumia vyakula vya uwanga ujazo wa mkono , mboga mboga Kwa wingi na mafuta yasiozidi vijiko viwili vya chakula, tuwe na  Utamaduni huu ili kupunguza ongezeko la maradhi haya".Alifahamisha dkt. Hafidh.
Kuanzishwa kwa vikundi vya maradhi yasioambukiza vijijini ni mpango wa Wizara ya Afya wa kuweza kuwasogezea huduma za Afya wenye maradhi hayo  katika ngazi ya jamii wakishirikiana na Pharm Access.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.