Habari za Punde

ZAFICO Waunga Mkono Jitihada za Waanika Dagaa Kama Unguja

Mkurugenzi mwendeshaji kampuni ya uvuvi Zanzibar (ZAFICO) dkt. Ameir Haidar Mshenga akitiliana saini na Mkuu wa Idara ya uchumi na uzalishaji Jeshi la Kujenga Uchumi JKU   Kanal Jabir Saleh Simba   hati ya makubaliano ya ujenzi wa mradi wa chanja za kuanikia dagaa  kwaajili ya wajasiriamali wanaoanika madagaa eneo la Kama,hafla iloyofanyika Kama Wilaya ya Magharibi A Mkoa wa mjini Magharibi.

Na Fauzia Mussa -Maelezo Zanzibar.

Wajasiriamali  wadogo wadogo wanaoishi Kama na vijiji jirani wanatarajiwa kunufaika na mradi wa ujenzi wa chanja za kuanikia dagaa utakaoanza hivi karibuni huko Kama wilaya ya Magharibi A.

Akingumza mara baada ya utiaji saini   kati ya kampuni ya Uvuvi Zanzibar (ZAFICO) na  Jeshi la Kujenga Uuchumi (JKU) Mkurugenzi mwendeshaji wa kampuni hiyo dkt Ameir Haidar Mshenga amesema mradi huo utaisaidia Serikali katika kuhakikisha wananchi wanajiendeleza kiuchumi na kupunguza  wimbi la vijana wasio na ajira.

Amesema vijana wengi wamekua wakijiingiza katika vikundi viovu kwa kisingizio cha kukosa  ajira  hivyo mradi huo utawawezesha vijana kujiajiri na kujiongeza kipato huku akiwaomba  wananchi waishio vijiji jirani kujitokeza kunufaika namradi huo ili kujiletea maendeleo.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya uchumi na uzalishaji Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) Kanal Jabir Saleh Simba amefahamisha kuwa ujenzi huo unatarajiwa  kuanza hivi karibuni na kuwahakikisha wananchi kukamilika kwa wakati kwa kuzingatia viwango.
Nao wananchi wanaotarajiwa kunufaika na mradi huo wamewataka Vijana kuacha kukaa katika makundi yasiofaa (maskani) na badala yake kujiunga na vikundi vya ujasiriamali ili kujipatia kipato cha halali na kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha vijana wote wanajiajiri .

Aidha  waliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa juhudi wanazozifanya za kuhakikisha wananchi wote  wanafanya kazi na kuweza kukidhi mahitaji yao.

Mradi huo utagharimu zaidi ya bilioni mbili ambapo  utajumuisha eneo la kukoshea,kuanikia na sehemu ya baridi kuweza kusaidia wajasiria Mali kuhifadhi dagaa endapo litapatikana kwa wingi.


Mjasiriamali wa kuanika dagaa na mkaazi wa Kama Khamis khamis vuai akiuliza suali kwa kanal Jabir Saleh Simba kuhusiana na muda wa  kumalizika kwa mradi wa  wa chanja za kuanikia dagaa  mara baada ya kutiliana saini na Kampuni ya Uvuvi Zanzibar ZAFICO hati za ujenzi huo huko Kama Wilaya ya Magharibi A Mkoa wa mjini Magharibi.
Mkuu wa Idara ya uchumi na uzalishaji Jeshi la Kujenga Uchumi JKU   Kanal Jabir Saleh Simba akijibu swali la mwananchi lililokua likihusiana na muda wa kumalizika kwa mradi wa chanja za kuanikia dagaa  ambapo amesema mradi huo utanza hivi karibuni na kuchukua  muda wa mezi minnehadi kukamilika ,hafla hiyo  iliyofanyika Kama Wilaya ya Magharibi A Mkoa wa mjini Magharibi.juni 07,2023.PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANZIBAR .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.