Habari za Punde

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan azindua Mkongo wa Mawasiliano wa Baharini wa 2Afrika pamoja na Teknolojia ya Mawasiliano ya Kasi ya 5G ya Kampuni ya Mawasiliano na Simu za Mkononi ya Airtel Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amevaa Kifaa Maalum cha kumuwezesha kuona kwa ukaribu matukio mbalimbali Duniani kijulikanacho kama Teknolojia Ukweli Halisi (Virtual Reality Device) mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Mkongo wa Mawasiliano Baharini cha Kampuni ya Airtel Tanzania kilichopo Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023. Wengine katika picha ni Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye pamoja na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano na Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania Dinesh Balsingh wakishuhudia tukio hilo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wengine wakati akimsikiliza Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye kuhusu Mkongo wa Mawasiliano wa Baharini wa 2Afrika kabla ya kuuzindua katika Kituo hicho cha Kampuni ya Mawasiliano na Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania kilichopo Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye wakati akielekea kuzindua Kituo cha Mkongo wa Baharini cha Airtel 2Afrika cha Kampuni Mawasiliano na Simu za mkononi ya Artel Tanzania kilichopo Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati wakimuangalia Msanii Mrisho Mpoto alipokuwa akitumbuiza kwenye kwenye hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mkongo wa Baharini cha Airtel 2Afrika pamoja na Mtandao wenye kasi ya 5G wa Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania iliyofanyika Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wadau wa Mawasiliano kwenye hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mkongo wa Baharini cha Airtel 2Afrika pamoja na Mtandao wenye kasi ya 5G wa Kampuni ya Mawasiliano ya Artel Tanzania iliyofanyika Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kuashiria uzinduzi wa Mtandao wenye kasi ya 5G wa Kampuni ya Airtel Tanzania katika hafla iliyofanyika  Kituo cha Mkongo wa Mawasiliano Baharini cha Kampuni ya Airtel Tanzania kilichopo Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwa njia ya Mtandao na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mkongo wa Baharini cha Airtel 2Afrika pamoja na Mtandao wenye kasi ya 5G wa Kampuni ya Mawasiliano ya Artel Tanzania iliyofanyika Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023.


 

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.