Habari za Punde

Wizara Itahakikisha Inawasimamia Kupata Haki Zao kwa Kuwachukulia Hatua Wale Wote Wanaofanya Vitendo Viovu Vya Udhalilishaji

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Zanzibar Bi. Abeida Rashid Abdalla akimkabidhi Cheti mmoja wa Washiriki wa Mafunzo yaliyolenga kuzuiya vitendo vya udhalilishaji Zanzibar, yaliyofanyika katika ukumbi wa Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja.  
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Zanzibar Bi. Abeida Rashid Abdalla akiwa na Wakufunzi wa Mafunzo ya kuzuiya vitendo vya udhalilishaji Zanzibar, wakiwapondeza Wanafunzi wakiimba wimbo maalum wa kupinga vitendo vya  udhalilishaji kwa Watoto na Wanawake yaliyofanyika katika ukumbi wa Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja.  
Wanafunzi wakiimba wimbo maalum wa kupinga vitendo vya  udhalilishaji kwa Watoto na Wanawake yaliyofanyika katika ukumbi wa Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja.  

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Zanzibar Bi. Abeida Rashid Abdalla akizungumza na kuyafungua mafunzo yaliyolenga kuzuiya  vitendo vya udhalilishaji Zanzibar, yaliyofanyika katika ukumbi wa Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja.  

Wazazi wametakiwa kuwa na mashirikiano ya kuwalea watoto  katika malezi bora ili kuwakuza kwenye  maadili mema yatakayowafanya kujitambua dhidi ya Vitendo vya Udhalilishaji na Ukatili wa kijinsia.

Akizungumza katika ghafla ya ufungaji wa mafunzo ya Kuzuia Vitendo vya Udhalilishaji Zanzibar huko Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ndugu Abeida Rashid Abdallah Wizara yake itahakikisha inawasimamia kupata haki zao kwa kuwachukulia hatua wale wote wanaofanya vitendo viovu.

Katibu Abeida amewataka Wazazi kutoa Ushirikiano na kuachana na tabia ya muhali pindi unapohitajika ushahidi mahakamani.

Mkurugenzi wa Mradi wa kuzuia Vitendo vya Udhalilishaji Zanzibar bwana Patrick Lemo Amesema la mradi huo ni kuelimisha Jamii dhidi ya kuwalinda watoto kunusurika na janga la kufanyiwa vitendo hivyo.

Pia amewataka Walimu na Wanafunzi waliopatiwa mafunzo hayo kuwafikishia wengine sambamba na kuiomba Serikali kuwasaidia ili kutoa Elimu hiyo kwa mikoa yote ya Unguja.

Akisoma Risala kwa niaba ya watoto waliopatiwa mafunzo hayo Aisha Machano Yussuf amesema mafunzo waliyopatiwa yamewapa mwanga wa kuelewa hatua hatua za kuchukua pindi wanapohisi dalili za mtu anapotaka kuwafanyia vitendo viovu pamoja na kuiomba jamii na taasisi husika kushirikiana kwa pamoja katika kuzuia vitendo vya udhalilishaji

Mafunzo hayo ya miezi Minne yenye dhima ya kuelimisha jamii dhidi ya vitendo vya vya Udhalilishaji wa kijinsia kwa watoto yamesimamiwa na Shirika la Path finder, C Sema, Action Aid na ICRW.

Mwisho

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.