Habari za Punde

Mkutano wa Wakuu wa Taasisi za SMT na SMZ (CEOs) Wafanyika Zanzibar Katika Kusherehekea Miaka 6O ya Mapinduzi ya Zanzibar

Naibu waziri wa Viwanda na Biashara WA Serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania Exaud Kigahe akizungumza wakati akifungua mkutano wa wakuu wa Taasisi za SMZ na SMT katika kusherehekea miaka 60 ya Mapinduzi,Hafla iliyofanyika Ukumbi wa Dkt Hussein Mwinyi kituo cha maonesho ya Biashara nyamazi Zanzibar.

 Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Exaud Kigahe amezitaka Taasisi zinazohusika na Biashara kuendelea  kutoa Elimu kwa wananchi ili kujenga  uwelewa juu ya  biashara.

"Sisi wa Tanzania tunategemea biashara hivyo tujitahidi kufahamu umuhimu wa biashara na tuondoe malalamiko" alisisitiza.,Naibu Waziri wa 

 

Ameyasema hayo katika Ukumbi wa Dkt Mwinyi Nyamanzi Wilaya Magharib B' katika ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Taasisi za SMT na SMZ katika kusheherekea miaka 60 ya Mapinduzi.

 

Amesema wafanya biashaa wengi hawana uwelewa juu ya makato na tozo za biashara kati ya Zanzibar na Tanzania jambo linalopelekea malalamiko hivyo ipo haja kwa taasisi husika kuendelea kutoa elimu ya kuwajengea uelewa dhidi ya malalamiko hayo.

 

Aidha amefahamisha  kuwa kuna changamoto nyingi katika Taasisi za biashara  hivyo ni vyema kukaa pamoja nakushirikiana  kuzitatua changamoto hizo ili kutoa fursa kwa wafanya biashara kuendelea na  biashara zao pamoja  na kuleta maendeleo.

 

Ameeleza kuwa ikiwa wanakaribia kufikia miaka 60 ya Muungano wa Tanzania amezitaka  Taasisi husika Kuwasaidia Sekta Binafsi ili kuweza kutoa mchango wao katika biashara.


"Sisi tuna haja ya kusimamia na kutekekeza malengo ya biashara ili kuleta mafanikio yetu katika muungano wetu" alisema 


Ameongeza kuwa Tanzania Bara na Zanzibar ni nchi moja hivyo ni vyema kushirikiana kwa pamoja ili kuleta mafanikio kwa pande zote mbili.


Aidha amewashukuru Marais wa Serikali zote mbili kwa kazi kubwa wanazozifanya ya kuleta maendeleo nchini.


Nae Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe Rashid Salim amesema kuwa kikao hicho kitasaidia kujenga mashirikiano zaidi, kujifunza pamoja na kubadilishana uzoefu.

 

Aidha ameeleza kuwa kikao hicho pia kitatoa fursa kwa watendaji wa Taasisi hizo kufikia malengo katika utendaji wa kazi zao.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wakuu wa Taasisi Latifa Khamis  amefahamisha kuwa jukwaa hilo limeanza mwaka 2016 kwa lengo la kukuza ushirikiano ili kupanua ukuaji wa uchumi wa Tanzania.


Amesema kuwa kikao hicho kina  lengo la kutekekeza malengo ya miaka 60 ya Mapinduzi  ambayo yana mafanikio makubwa .


Aidha amefahamisha kuwa  tangu kuanzishwa kwa jukwaa hilo wamefanikiwa kubadilishana uzoefu na kukubaliana katika mambo  mbali mbali ya kuimarisha utendaji wa majukumu yao.


Nao washiriki wa mkutano huo wamesema kuwa wataendelea kushirikiana baina yao  kwa kufanya kazi kwa pamoja ili kufikia malengo yayaliyokusudiwa.


Katika Makutano huo Taasisi mbali mbali za SMZ na SMT zilishiriki ikiwemo TANESCO, TRA, ATC, TPA, LATRA na TASAC.


Mwenyekiti wa jukwaa la Taasisi za SMZ na SMT  (CEOs)  Latifa M.Khamis akitoa maelezo mafupi kuhusiana na umoja huo katika mkutano wa wakuu wa Taasisi hizo uliofanyika katika Ukumbi wa Dkt Hussein Mwinyi Nyamanzi katika kusherehekea miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Naibu katibu mkuu Wizara ya biashara na maendeleo ya Viwanda Zanzibar Rashid A. Salim  akimkaribisha Naibu waziri wa Viwanda na Biashara WA Serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania Exaud Kigahe  kifungua mkutano wa wakuu wa Taasisi za SMZ na SMT katika kusherehekea miaka 60 ya Mapinduzi huko Ukumbi wa Dkt Hussein Mwinyi eneo la maenesho ya Biashara nyamazi Zanzibar. 
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.