Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Amezindua Jezi ya Timu ya Taifa ya Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisaini  moja ya Jezi Mpya za Timu ya Taifa ya Zanzibar Zanzibar Heroes, wakati wa uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Viwanja vya Maonesho Nyamazi Wilaya ya Magharibi "B" Unguja 26-1-2024  na (kulia kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema jezi alizozindua zitatumika katika mashindano ya uwakilishi  wa nchi ndani na nje katika michuano ya madaraja mbalimbali. 

Rais  Dk.Mwinyi  amesema hayo alipozindua  rasmi Jezi za Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) tarehe: 26 Januari 2024 katika Viwanja vya maonesho Nyamanzi Mkoa wa Mjini Magharibi. 

Aidha Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa changamoto ya Zanzibar kushiriki michuano inayoandaliwa na Shirikisho la mpira Afrika(CAF) ikiwemo michuano ya AFCON inaelekea kupatiwa ufumbuzi kupitia Wizara ya Michezo  kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF).

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amempongeza mbunifu wa mavazi nchini Sheria Ngowi kwa ubunifu wa jezi hizo .

Pia ameishukuru benki ya CRDB kwa kuona umuhimu kuunga mkono jitihada za Serikali katika michezo.

Vilevile Serikali inayo azma ya kufundisha makocha nchini pamoja na kuhamasisha uendelezwaji na kuanzishwa kwa academia za michezo katika kuandaa timu bora ya Taifa  kwa uwakilishi wa Kikanda na Kimataifa. 

Halikadhalika  Rais Dk.Mwinyi ametoa wito kwa taasisi zinazolinda haki miliki kulinda jezi hizo pia kuchukua hatua za kisheria kwa  mtu yeyote atakayebainika kutengeneza jezi hizo bila ridhaa au kibali maalum kutoka ZFF.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.