Habari za Punde

(ORKSUU) Yawasilisha Taarifa ya Utekelezaji kwa Kipindi cha Januari hadi March 2024 kwa Kamati ya B.L.W

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Mhe Haroun Ali Suleiman akisoma taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi hiyo kwa kipindi Cha January -machi 2024 mbele ya Kamati ya kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa kitaifa ya Baraza la wawakilishi, hafla iliyofanyika Chukwani Zanzibar.

Mwenyekiti wa Kamati ya kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa kitaifa ya Baraza la wawakilishi Mhe. Machano Othman Said akizungumza na watendaji wa Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora mara baada ya kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi hiyo kwa kipindi Cha January - Machi 2024.

PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR 

Na Fauzia Mussa. Maelezo. 03.04.2024.

Mwenyekiti wa Kamati ya kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa kitaifa ya Baraza la wawakilishi Mhe. Machano Othman Said ameitaka Ofisi ya mwendesha mshtaka, Mahakama, Mwanasheria mkuu na Zaeca kuendelea kushirikiana ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.


Ameyasema hayo mara baada ya kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora kwa kipindi Cha January - Machi 2024 huko katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi ‘’B’’.


Amesema Taasisi hizo zinabeba dhamana kubwa ya wananchi ikiwemo haki za watu na maisha yao hivyo iwapo zitashirikiana na kufanya kazi kwa pamoja wataweza kufikia malengo ya kutoa huduma bora kwa wananchi.


"Wakati nwengine kuna malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa kesi zinachelewa na kesi zikichelewa ndio unamnyima mtu haki yake, au uchunguzi wa kesi unachelewa kwa hiyo huu ni mnyororo ni vyema mnyororo huu kushirikiana zaidi ili kufikia malengo yaliyokisudiwa".


Aidha ameizishukuru Taasisi za kidini ikiwemo Ofisi ya mufti mkuu wa Zanzibar na kadhi mkuu wa Zanzibar kutokana na mabadiliko yao makubwa katika utendaji na kuwaomba kuendelea kufanya kazi kwa pamoja na kuwataka kumaliza changamoto za wakfu ikiwemo mashamba, majengo na mambo mengine ili kuondosha migogoro katika jamii.


Kwaupande wake Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman amesema katika kipindi cha Januari hadi Machi,2024, Ofisi hiyo imesimamia na kutekeleza shughuli mbali mbali za Sekta ya Sheria, na inaendelea na uratibu wa Mradi wa Uwezeshaji na Upatikanaji wa haki-Awamu ya Pili kwa mwaka 2024.


Aidha amesema Ofisi inaendelea kutoa mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo 

Wapelelezi na Waendesha Mashtaka ili kuweza kupeleleza na kuendesha kesi za 

aina hiyo Ili kutatua changamoto ya Uhaba wa taaluma na ujuzi mahsusi kwa Waendesha Mashtaka na Wapelelezi wa makosa ya udhalilishaji na uhalifu wa kupangwa wa kiuchumi.


Aidha Ofisi ya Rais inawapatia mafunzo ya uchunguzi na vifaa watendaji wa Mamlaka kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kuendesha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali za rushwa na uhujumu Uchumi.

Hata hivyo amesema Ofisi ya raisi imejipanga Kuimarisha upatikanaji wa haki na utawala wa sheria, kusikiliza kesi na kutoa maamuzi ya haraka na kwa wakati, pamoja na kuhakikisha Upatikanaji wa Msaada wa Kisheria katika maeneo yote ya kijamii.


Nao Wajumbe wa kamati hiyo wameiomba Ofisi ya mufti mkuu wa Zanzibar kutoa elimu kwa walimu wa madrasa ili kuondoa wimbi la vitendo vya udhalilishaji vinavyoonekana kuongezeka siku hadi siku.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.