Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa rai kwa Wasomi, wanazuoni wenye taaluma, maarifa na uzoefu wa
masuala mbalimbali ya taaluma, kujadili fursa na changamoto zilizopatikana
ndani ya kipindi cha miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanziabar na Muungano wa Tanzania
hasa kwenye utekelezaji wa Sera na Mipango ya Serikali.
Rais Dk. Mwinyi pia aliwasihi wasomi hao kutumia fursa za
majukwaa na makongamano ya taaluma kuzungumzia Sera zinazopewa kipaumbelee na Serikali
zote mbili za Mapinduzi ya Zanzibar na ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika utekelezaji wa Mipango mikuu
ya nchi ikiwemo Uchumi wa Buluu, Uwekezaji, Diplomasia ya Uchumi pamoja
na kutoa mapendekezo yenye kuboresha ustawi wa Taifa.
Dk. Mwinyi ameyasema hayo kwenye
ukumbi wa Dk. Ali Muhammed Shein, Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja
alipofungua Kongamano la kitaaluma la kumbukumbu ya miaka 60 ya
Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, liliandaliwa na Baraza la Uongozi na
Menejimenti ya Chuo cha Utumishi wa Umma - Zanzibar (IPA) na Baraza la Uongozi
na Menejimenti ya Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim (CFR)
kutoka Kurasini - Dar es Salaam
Alisema, miaka 60 ya Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar na Muungano wa Tanzania, ni chachu ya maendeleo mengi
yaliyopatikana kutoka sekta mbalimbali za Uchumi, Jamii, Siasa na Diplomasia.
Pia Rais Dk. Mwinyi alieleza
imani yake kwa wataalamu wabobezi wakiwemo wasomi na wanzuoni kwenye Kongfamno
hilo, kuendelea kuelezea faida na matunda ya Mapinduzi, Muungano na Umoja wa
Watanzania sambamba na kutoa hoja madhubuti, takwimu na maelezo ya kina
yatakayolitambulisha vyema taifa hasa kwa nyakati zilizopita wakati uliopo na
unaokuja.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi alivipongeza
vyuo vya Utumishi wa Umma, Zanzibar (IPA) na Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha
Dkt. Salim Ahmed Salim (CFR) kwa mpango wa kuendesha shindano la uandishi wa
insha lenye lengo la kuimarisha kumbukumbu ya miaka 60 ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar na Mapinduzi Matukufu za Zanzibar kwa wanafunzi wa Skuli
zote za Msingi na Sekondari nchi nzima.
Halkadhalika, Rais Dk. Mwinyi aliwanasihi washiriki wa
Kongamano hilo, kuitumia vizuri fursa hiyo kwa kujadili
umuhimu wa kudumisha Mapinduzi ya Zanzibar na kuuenzi Muungano wa Tanzania kwa
dhamira ile ile ya Waasisi wa Taifa, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume na Hayati
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Vile vile, Dk. Mwinyi alitoa wito kwa washiriki wa Kongamano hilo, kutumia vyema
jukwaa hilo kwa kuchangia na kutoa maoni yenye lengo la kuimarisha na kujenga manufaa
zaidi yanayotokana na tunu za Mapinduzi na Muungano kwa Taifa kwani ndio msingi wa kuendelea kuwepo
kwa hali ya amani, usalama na Umoja wa Kitaifa.
Akizungumza kwenye kongamano
hilo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Haroun Ali
Suleiman pia aliwataka washiriki wa Kongamano hilo kuendelea kuhubiri juhudi
kubwa zinazoendelea kufanywa na viongozi waliopo madarakani, Dk. Samia Suluhu
Hassan an DK . Husssein Ali Mwinyi ya kuendelea kuhubiri amani, utulivu na
ushirikiano baina ya Wa Tanzania.
Naye, Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Januari Yussuf Makamba amewapongeza
Wanzibari na Wanatnzania kwa ujumla hasa kwa ushiriki wao wa moja kwa moja kwa
kujadili Sera mpya ya Mambo ya nje ambayo pia imejumiya masuala ya Uchumi wa
Buluu yenye tija kubwa kwa ustawi na
maendeleo ya utalii nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Baraza la Uongozi na Menejimenti ya Kituo cha Uhusiano wa
Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim (CFR) kutoka Dar es Salaam, Balozi
Ramadhan Muombwa Mwinyi amesema wameamua kushirikiana na IPA kuandaa Kongamano
hilo kwa lengo la kuwaweka pamoja Watanzania ili kujadili mchango wa Diplomasia
na Sekta ya Umma kwenye maisha yao ya elimu na kuongeza uelewa kwa wananchi
hasa kwa masuala mbalimbali ya uchumi na mandeeo kwa ustawi wa taifa lao la
Tanzania
Sambamba naye, Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma -
Zanzibar (IPA), Dr. Shaaban Mwinchum Suleiman, ameiomba Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kukiboresha chuo hicho na kukiongeza hadhi kwa kuwajengea
jengo jipya litakaloimarisha huduma zao, Ombi lililokubaliwa na Serikali.
Kongamano la kitaaluma la
kumbukumbu ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar, lenye kauli mbiu isemayo “Miaka 60 ya Muungano katika
diplomasia na Maendeleo Endelevu ya Uchumi wa Buluu”.
No comments:
Post a Comment