Habari za Punde

Waziri Mhagama ahimiza utunzaji wa Mazingira Songea

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Morogoro kilichopo Halmashauri ya wilaya ya Songea.
Wananchi wa Kijiji cha Morogoro Wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho (Hayupo pichani) katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji hicho. 

Na Mwandishi wetu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho ameendelea kuhimiza wananchi kuhimiza wananchi kutunza mazingira na kuachana na tabia ya kukata miti hovyo ili kuepukana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Waziri ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara iliyofanyika katika vijiji vya Nakauga na Morogoro vilivyopo katika kata ya Litisha Halmashauri ya wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma leo tarehe 17/07/2024.

“Niwaombe wananchi kila mtu awe mlinzi wa mwengine ili kuhakikisha mazingira yanatunzwa, ni bora kupanda miti kuliko kukata miti, tupande miti mingi ya matunda na hii iwe kampeni maalumu,” alisema Waziri Mhagama.

Naomba pia tuanze kupunguza matumizi ya kuni ambayo yanaendelea kuharibu mazingira, Mhe. Rais anataka wanawake tuanze kutumia nishati safi ya kupikia.

“Huko tunakoelekea mitungi ya gesi mkaa rafiki unaotokana na makaa ya mawe na majiko ya umeme yanayotumia umeme kidogo vitapatikana kwa urahisi hivyo itatoa nafasi ya wakinamama kuchagua anachotaka kutumia ili kuepukana na kadhia ya kuharibu mazingira,” alieleza.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa wilaya ya Songea Ndg. Mtela Mwampamba amesema kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya Maafisa Watendaji wa Vijiji na Wenyeviti wa vijiji kuuza maeneo ya vijiji kiholela.

“Sheria ya ardhi ya Kijiji ya Mwaka 1999 sheria no 4 inaeleza kwamba miliki yote ya ardhi ya kijiji itamilikiwa na kusimamiwa na Mkutano Mkuu wa Kijiji na si viongozi wa kijiji,“ alisema Katibu Tawala Mwampamba.

Ameeleza viongozi wa kijiji watatumika kama wawakilishi katika usimamizi wa ardhi ya kijiji na hawaruhusiwi kuuza au kugawa eneo la ardhi ya kijiji bila Mkutano Mkuu wa kijiji kutoa uamuzi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.