Afisa Usimamizi wa Fedha Mwandamizi wa Wizara ya Fedha, Bi. Mary Mihigo, akitoa elimu ya fedha kwa wananchi kuhusu umuhimu wa usimamizi wa fedha binafsi, jinsi ya kupanga mapato na matumizi ili kuweka akiba na kujikwamua kiuchumi pamoja na kujiandaa na maisha ya baadaye, wakati Maafisa wa Wizara ya Fedha walipokuwa wakitoa elimu ya fedha kwa wananchi katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Chalinze.
Afisa Usimamizi wa Fedha Mwandamizi wa Wizara ya Fedha, Bi. Mary Mihigo, (mwenye sare), akijadiliana na wananchi mbinu za kuhakikisha mikopo wanayochukua ni salama kwa kuzingatia taasisi za watoa huduma za fedha zilizosajiliwa, wakati Maafisa wa Wizara ya Fedha walipokuwa wakitoa elimu ya fedha kwa wananchi, katika Kata ya Kiwangwa, Halmashauri ya Chalinze.
Na. Saidina Msangi, Chalinze, Pwani.
Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze wameishukuru Serikali kwa kuwafikishia elimu ya fedha itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi kwa kutumia fursa za uwekezaji ili kujiongezea kipato na kuongeza thamani ya akiba zao.
Wananchi hao walitoa shukrani hizo baada ya kupata mafunzo ya elimu ya fedha yaliyoratibiwa na Wizara ya Fedha, yenye kauli mbiu "Elimu ya fedha ni msingi wa maendeleo ya kiuchumi" ambayo yametolewa kwa siku mbili katika ukumbi wa mikutano wa Wilaya ya Halmashauri ya Chalinze.
Akizungumza kwa niaba ya washiriki wenzake, Bi. Mery
Leonard Chiwiko, aliishukuru Wizara ya Fedha kwa kuwapa
elimu hiyo muhimu, akisema kuwa hapo awali hawakuwa na
uelewa mzuri kuhusu masuala ya fedha, mikopo na uwekezaji.
"Tunaishukuru Wizara ya Fedha kwa kutupatia elimu hii,
itatusaidia sana katika kuimarisha maisha yetu ya kifedha,
kuepukana na mikopo umiza na pia tumejifunza kuwa hata
kama una kipato kidogo inawezekana kuweka akiba na
kuwekeza akiba hiyo na kupata faida," alisema Chiwiko.
Wananchi hao waliiomba Serikali kuona namna ya
kuwafikishia mafunzo ya elimu ya fedha ikiwezekana mara
mbili kwa mwaka kutokana na umuhimu wake katika
kuwawezesha kukabiliana na changamoto za kiuchumi.
Timu ya Maafisa kutoka kutoka Wizara ya Fedha imetoa
mafunzo ya elimu ya fedha ikiwemo namna ya kuweka akiba
na mbinu za usimamizi wa fedha na uwekezaji kwa washiriki
zaidi ya 800 ambao wanatarajiwa kuwa mabalozi wa
kuwafikishia wenzao elimu hiyo ili nao waweze kunufaika na
kujikwamua kiuchumi.
No comments:
Post a Comment