Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Azungumza na Mwanazuoni Dr. Zakir Naik Ikulu Zanzibar

Raus wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Mwazuoni Dk.Zakir Naik, (kulia kwa Rais) alipofika Ikulu na Ujumbe wake kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar na (kushoto kwa Rais) Mufti Mkuu wq Zanzibar Mhe. Sheikh Saleh Omar Kabi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema  dhana ya  Utalii wa Maadili inaendelea kukua zaidi kufuatia Ujio wa Viongozi  mbalimbali wa Kiimani  nchini.

Rais Dk.Mwinyi  ameyasema hayo alipozungumza na Mwanazuoni  Dk, Zakir Naik wa Taasisi ya  Putrajaya ya Malaysia na Ujumbe wake waliofika Ikulu kuonana naye.

Aidha Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa  Zanzibar Imekuwa na fursa kubwa  ya kuendeleza Utalii na ajira kwa Vijana kufuatia utekelezaji wa dhana hiyo ya utalii wa Maadili  iliokubalika na  jamii

Rais Dk.Mwinyi amemsisitiza Mwanazuoni huyo kuyatembelea Maeneo zaidi ya Kihistoria yaliopo nchini na kuwa Balozi wa Kuitangaza Zanzibar Kimataifa.

Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi  amemshauri Dk.Zakir  kufikiria Kuitembelea Zanzibar Kipindi cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani  kwa lengo la kufanya Mihadhara kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu.

Naye Dk.Zakir Naik  amesifu Maendeleo  yanayofikiwa nchini  pamoja na  muendelezo Mzuri wa  harakati za Dini ya Kiislamu hapa nchini na kuahidi ushirikiano.







No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.