Mkutano huo wa siku tano kuanzia Februari 10 hadi 14, 2025 utafanyika katika ngazi tatu; ngazi ya Wataalamu tarehe 10 -12 Februari 2025, ngazi ya Makatibu Wakuu tarehe 13 Februari 2024 na kuhitimishwa katika ngazi ya Mawaziri tarehe 14 Februari 2025.
Mkutano huo unatarajiwa kupokea na kujadili taarifa mbalimbali za maendeleo ya sekta ya nishati, petroli na madini katika Jumuiya na kuweka mikakati ya pamoja ya kutatua chagamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo ili kuhakikisha nchi wanachama wananufaika kutokana na mchango wa sekta hizo, vilevile kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu na endelevu katika Jumuiya.
Ili kufikia adhima hiyo mkutano huo utaangazia agenda
mbalimbali ikiwemo; hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa
maamuzi ya baraza la hilo la sekta, matumizi ya nishati safi,
salama na ufanisi wake, Mkutano na Maonyesho ya 11 ya
Petroli ya Afrika Mashariki yanayotarajiwa kufanyika jijini
Dar es Salaam tarehe 5-7 Machi 2025 na kuhuisha taarifa za utekelezaji wa miradi ya kuunganisha na kusambaza nishati katika Jumuiya.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo wa ngazi ya
wataalamu Mkurugenzi wa Sekta za Uzalishaji wa Sekretariati
ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Jean Baptiste
Havugimana ameeleza kuwa licha ya mafanikio yaliyofikiwa
katika sekta hiyo bado mchango na weledi wa wataalamu wa
sekta hizo muhimu katika kukuza uchumi wa Jumuiya
unahitajika ili kutatua changamoto zilizopo na hatimaye
kufikia malengo yanayotarajiwa na Jumuiya.
Havugimana ametoa rai kwa watalamu hao kujikita katika
kujadili na kuyapatia ufumbuzi wa kudumu masuala muhimu
yatakayojili katika mkutano huo kwa manufaa ya Jumuiya.
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo wa ngazi ya wataalamu unaongozwa na Bw. Abdillah Mataka Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mkutano huo unaotarajiwa hutimishwa tarehe 14 Februari 2025 katika ngazi ya Mawaziri wanaosimamia sekta ya nishati, petroli na madini umehudhiriwa na wajumbe kutoka Nchi zote saba (7) wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment