WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Mhe. Ali Suleiman Ameir (Mrembo) akizungumza na Kaimu Balozi wa Saudi Arabia Nchini Tanzania Mhe. Abdallah Al Kashami, wakati wa mazungumzo hayo yaliyofanyika Ofisini Kwake Ikulu Zanzibar, kabla ya kukabidhiwa msaada wa tende iliyotolewa na Mfalme wa Saudi Arabia
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Ikulu Ali Suleiman Ameir amesema Zanzibar inathamini Mchango na Misaada ya Kijamii katika nyanja mbalimbali inayotolewa na Saudi Arabia inayosaidia Kuimarisha Ustawi wa jamii kwa Wananchi.
Waziri Ameir ametoa Tamko Hilo alipozungumza na Kaimu Balozi wa Saudi Arabia Tanzania Abdalla Alkashami akiambatana na Ujumbe wake Waliofika Ikulu kukabidhi zawadi ya Tani 25 za Tende kwa ajili ya Wananchi wa Zanzibar iliotolewa na Mfuko wa Mfalme wa Nchi Hiyo Salman Abdulaazizi
Ameeleza kuwa Serikali imepokea zawadi Hiyo na kuishukuru Nchi Hiyo kwa kuichagua Zanzibar kuwa Miongoni mwa Nchi zinazostahiki Kupata zawadi Hiyo ambayo tayari imeanza kugaiwa kwa Wananchi katika Maeneo mbalimbali.
Aidha ameuhakikishia Ujumbe huo kuwa Zanzibar itaendeleza Ushirikiano wa Muda mrefu Uliopo Baina ya Nchi hizo ambayo umekuwa na Manufaa kwa Pande zote mbili.
Naye Kaimu Balozi Abdalla Alkashami amesema Utaratibu huo wa kila Mwaka unatekelezwa na Mfuko wa Mfalme wa Saudi Arabia ikiwa ni hatua ya Kuimarisha Ushirikiano na Upendo na kuishukuru Zanzibar kwa kupokea Tende hiyo.
No comments:
Post a Comment