Habari za Punde

MCHANGO WAKO UNAHITAJIKA KWA AJILI YA UJENZI WA MSIKITI

Hii ni kuwapa taarifa Waislamu popote walipo katika ardhi hii ya Allah Subhaanahu Wata’ala kuanza kujitengenezea kijiakiba ambacho kitakachoweza kuwafaa baada ya kutangulia kwenye haki. Watakaokuwa na uwezo wa aina yoyote katika kufanikisha amali hii ya kheri basi tunawaomba waanze kujitayarisha kwani Allah Subhaanahu Wata’ala Anasema katika Qur'aan

Hakika wanaoamirisha Misikiti ya Allah Ni wale wanaomuamini Allah Na Siku ya Mwisho, Na wakasimamisha Sala, Na wakatoa Zaka, na wala hawamuogopi ila Allah. Basi huenda hao wakawa katika waongofu. Attawbah/18

Na Mtume Swalla Allahu ‘Alayhi Wasallam Anasema katika Hadithi:
"Mwenye kujenga Msikiti kwa ajili ya Allah Subhaanahu Wata’ala, Allah Subhaanahu Wata'ala atamjengea nyumba peponi". Bukhaari

Uongozi wa Masjid Munawwar Jang'ombe kwa Maharuki - Zanzibar, unawatangazia Waislamu wote popote walipo kuchangia katika upanuzi wa Msikiti huu kwa kuwasilisha michango yao moja kwa moja Msikitini au kupitia

Benki ya watu wa Zanzibar

A/C 0212 0602 8457
Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na uongozi kwa namba
0777 450 140/0777238 927
Wajazaakumu llaahu khayraa

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.