CHAMA CHA USHIRIKA UDURU WASHINDA KESI,SHAMBA LARUDISHWA RASMI
-
*Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mhe. Hassan Bomboko, amesema kuwa, shamba la Chama
cha Ushirika Uduru Makoa lenye ukubwa wa ekari 358 limepokelewa rasmi na
ch...
35 minutes ago
Mzee Mapara,
ReplyDeleteKwanza tunakushukuru kwa kazi yako nzuri ya kutuelimisha na kutuhabarisha kwa njia ya picha. Tumeona picha za uzinduzi wa kampeni ya CCM na CUF kule Unguja. Kwa kweli picha picha zilikuwa safi sana ile mbaya.Tunakushukuru kwa hilo.
Pia tumeona picha za uzinduzi wa kampeni za CCM Pemba nazo pia ziko safi. Lakini naona sijaona picha za uzinduzi wa CUF Pemba ambazo zilikuwa siku moja kabla ya uzinduzi wa CCM. Vipi hukupata wasaa wa kwenda au vipi?
Mdau
USA
Ahsante Mdau kutoka USA kwa kuonesha upeo wa kujali kazi hii ya kublog.
ReplyDeletePicha za kampeni ya Pemba sikubahatika kuzipata kwani sikupangwa kwenda kucover tukio hilo wala la CCM kwani za CCM nimezipata kutoka kwa Ramadhan Othman ambae ni mpiga picha wa Rais.
Hata hivyo tuliweka tangazo katika blog kwamba tunakaribisha habari, picha na matukio ya kampeni kutoka chama chochote cha siasa ila ima hatujabahatika kupokea picha kutoka sehemu yoyote isipokuwa CCM kupitia kwa mpiga picha wa Rais.
Kazi hii pia tunaifanya katika mazingira magumu kwani hutegemea Kompyuta ya kazini kupandisha picha na sina Kompyuta yangu mwenyewe wala hakuna msaada wowote kutoka sehemu yoyote kwa hivyo tutakachojaaliwa kupandisha tunawaomba wadau mtushukuru kwa hilo kwani kazi hii ya kublog kama huna zana zako mwenyewe kamili inakuwa ngumu na hasa kwa mazingira yetu.
Siku nyengine hujaribu kupandisha mara huduma ya mtandao imekorofisha au usubiri mpaka Kompyuta iwe haina kazi na kadhalika.
Ila tunajaribu kwenda hivyo hivyo mambo mdundo
Nafikiri Mdau umenielewa
Salaam Maalim Mapara,
ReplyDeleteNimekuelewa kuhusu lile suala la picha za ufunguzi wa Kampeni ya CUF Pemba.
I really appreciate what you do. Keep it up!
Kazi yako ni kazi ya kishujaa. Hatuna cha kukupa isipokuwa asante!
Mdau
USA.