Habari za Punde

Apigwa Faini 50,000 kwa Kuuza Kanda za Ngono

Na Zuwena Shaaban, PEMBA.

WIZARA ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, imempiga faini ya shilingi 50,000 mfanyabiashara wa kanda za CD, kwa kukiuka maadili ya biashara hiyo.

Wizara hiyo ilitoa adhabu hiyo, kupitia Bodi ya Sensa na Maonyesho, imetowa adhabu hiyo, kwa mfanya biaashara Khamis Bakar Said, baada ya kupatikana na kosa la kuuza kanda za ngono.

Ofisa Mdhamini Wizara ya Habari Pemba, Ali Nassor Mohammed, alisema Wizara imetowa adhabu hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 19 (1)na (2) ya sheria ya Zanzibar ya mwaka 2009.


Afisa huyo, alisema kwamba adhabu hiyo imetolewa baada ya vyombo husika kuridhika na kosa hilo pamoja na mfanyabiashara mwenyewe kukiri kosa hilo na kuahidi kutorudia tena kosa hilo.

Alisema mtu yoyote anaekwenda kinyume na sheria hiyo analazimika kulipa faini au kifungo cha miezi sita au adhabu zote kwa pamoja, kwa kosala aina hiyo.

Hata hivyo, amewataka wananchi kushirikiana na Wizara yake, ili kuhakikisha mila na desturi za Wazanzibari zinalindwa ipasavyo, na Wizara itahakikisha kuwa inaimarisha maadili ya Mzanzibari

Mara kadhaa serikali ya Zanzibar, imekuwa ikitoa tamko la kuitaka jamii kufuata maadili ya utamaduni wa kizanzibari, huku ikiwaonya wafanyabiashara kuacha kuingiza nchini kanda zinazopotosha wananchi zikiwemo za vitendo vya ngono.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.