Habari za Punde

Ajinyonga kwa Shati Hadi Kufa

Na Mwanajuma Mmanga

MTU mmoja akiwa amekutwa chooni akiwa ameshafariki baada ya kujinyonga kwa kutumia shati lake.

Tukio hilo lililotokea juzi majira ya saa 11:55 jioni eneo la Migombani, Prizi wilaya ya mjini unguja.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Kamishna Msaidizi wa Polisi Aziz Juma Mohammed amethibitisha tukio hilo na kumtaja marehemu kuwa ni Said Hamad Said (50) mkaazi wa Migombani.

Aidha Kamanda Aziz alisema sababu za marehemu kuchukua uamuzi wa kujinyonga hazifahamiki ingawa Polisi inaendelea na uchunguzi kuhusu kifo hicho.

Alisema marehemu hakuacha maelezo ya aina yoyote chanzo cha kuchukua uamuzi huo hakijajulikana kwani marehemu hakuacha ujumbe wowote wa kimaandishi lakini wakati wa uhai wake alikuwa analewa pombe na kuvuta bangi.

Marehemu huyo alikuwa akipenda starehe kwa kutumia ulevi wa kienyeji ambapo mara nyingi zinapofanyika operesheni za polisi hupambana na ulevi huo na madawa ya kulevya alikuwa akitiwa mikononi mwa Polisi.

Aidha tukio hilo alisema limegundulika na kipande cha sigara ya bangi kwenye mfuko wake wa suruali.

Alisema mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi hospitali kuu ya Mnazimmoja na kuonekana kifo chake kimesababishwa na kukosa kuvuta hewa baada ya kujikaba shingo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.