Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Nassor Salim Jazira, akizungumza na Wanamaskani ya Kachorora wakati wa kuwakabidhi TV kwa ajili ya kupata habari mbalimbali, makabidhiano hayo yaliofanyika katika ukumbi wa maskani hiyo.
Wanachama wa Maskani wa Kachorora Rahaleo wakimsikiliza Mwakilishi wa jimbo la Rahaleo wakati wa kukabidhi TV katika Maskani hiyo.
Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Nassor Salim Jazira, akimkabidhi TV Mwenyekiti wa Maskani ya CCM ya Kachorora Rahaleo Mohammed Mussa Faya, kwa ajili ya Vijana wa maskani hiyo, makabidhiano hayo yamefanyika katika maskani hiyo.
shame on u mwakilishi....i wish ningeweza nionane na wewe uso kwa macho ikisha nikupe tusi ulilokuwa hujawahi kulitarajia katika maisha yako aibu gani...mwakilishi mzima baada ya kutafuta vitu vya kufanya ili wananchi wakaondoka na umaskini ndio kwanza unawapa kitv cha chogo ili wapate kukaa zaidi hapo maskani wakazidi kuwa hawana akili CCM hebu hizi maskani ziuweni ndio zinazofanya wazanzibari kuwa wajinga.....au ndio mnafanya makusudi ili wawe wajinga kila siku ili mupate kuwatawala......aaaahhhhh inauma ndani ya roho, munachaguliwa kufanya mapinduzi ya ya maendeleo si kufanya watu wajinga, au kwa kuwa hamjasoma basi kila kitu munachokifanya kinakuwa cha kipuuzi
ReplyDeleteNamna hiyo! tunatakiwa tuonyeshe sasa tunataka nini na hatutaki nini!
ReplyDeletekwa namna hii..tutafika tuu!
Naam wanawalemaza wenziwao kwa vitu vya kipuuzi kama hivyo.Tatizo ni kukosa elimu endelevu.Ukimuambgalia huyo mwakilishi ana tumbo kama vile mja mzito na huyo mwenyekiti yu hoi bin taaban si afadhali angewapa pesa lau ya kula siku moja.
ReplyDeleteHizi picture tatu alizopiga huyu muheshimiwa ziko expensive kuliko hiyo tv. Mwakilishi msalie mtume.... Au ndio wajinga ndio waliwao.
ReplyDeletekitivii chenyewe kidogo ,nchi 12 kama ina fika ,haina hata dvd ,au muakilishi uliogopa kuwapa dvd wasije kuangaliya CD za uamsho ? tv yenyewe used ,mshahara wote unapeleka wapi au una nyumba ndogo ?kuweni mubunifu,wapeni vitu vya kuzalisha na kuleta maendeleo ,si mnarubuni watu kwa vitu vya kitoto,
ReplyDeleteTV VLETI PLAZMA zimejaa teleeeeeeee