· Ni lazima awajibike kisheria na sio kisiasa pekee
· Wadai Wazanzibari wanaoishi nje:
Na Geofrey Kimbitikiri
Friday, 27 July, 2012.
Wameelezea Wazanzibari hao kuwa kwa wakati
huu wa uwazi na ukweli, kujiuzulu kwake kulikuwa hakutoshi kwani makosa ya
jinai yametokea chini ya uongozi wake.
"Kwa kweli hajawajibika bado mpaka atakaposimama mahkamani na kuwaeleza
wote wale waliopoteza jamaa zao na ndugu zao kwanini meli iliachiwa kujaza watu
kuliko kiwango chake." Wameelezea Wazanzibari hao kwa uchungu sana
walipohojiwa kwa njia ya simu.
"Ilipozama meli ya mwanzo katika 2011
kwenye Nov-Dec mapendekezo kadhaa yalitolewa na Kamati iliyochaguliwa na Rais
Dr Shein, Kamati ambayo ilikaa mawiki tele Hoteli ya Bwawani kuifanya kazi
hio.
Waziri Hamad alishindwa kuyasimamia
mapendekezo hayo, yaani alishindwa kazi yake.
Moja katika mapendekezo hayo ya
Kamati ya mwanzo ni kuwa alitakiwa Waziri ahakikishe kuwa meli hazijazi abiria
zaidi ya kiwango. " Waliendelea Wazanzibari hao huku wengine wakilia kwenye simu.
"Ni kweli Waziri Hamad asingeliweza
kuizuwia hali ya hewa kuchafuka au kuzuwia kasi ya mawimbi ya bahari ya Chumbe,
lakini kama boti ile ingelikuwa na abiria 250 tu ambao ndio kiwango chake basi
msiba ungelikuwa mdogo kwa wananchi kuliko ulivyokuwa hivi sasa."
Waliendelea Wazanzibari hao.
Wazanzibari hao wanakusudia kwa pamoja
kupeleka Mahkama Kuu ya Zanzibar ‘a class-action lawsuit’ dhidi
ya Bw. Hamad, ambayo itamtaka awalipe ndugu wa Wazanzibari wote waliopoteza
maisha yao na wale walioumia kwenye hili balaa, kwasababu wanasema yeye
anahusika moja kwa moja.
Pia, wanaeleza kuwa kama Bw. Hamad angelisimamia
vizuri usafiri wa meli baina ya Bara na Visiwani kama alivyotakiwa na ile
Kamati ya Rais basi maafa yaliotokea yasingelikuwa makubwa hivyo.
Wazanzibari hao wanastaajabu vipi baada ya
kuelezwa na Kitivo Cha Hali ya Hewa cha DSM kuwa bahari itakuwa chafu boti
ndogo kama hii ya MV Skagit iliweza kuruhusiwa kuanza safari yake na huku ikiwa
imechukuwa watu zaidi ya kiwango chake. “ Hii ni miradi ya wakubwa na kama boti
isingelisafiri watu wangelikosa sehemu yao”, walichacharika Wazanzibari hao.
Wazanzibari hao walivyoulizwa watadai kiasi
gani walipwe kwa kila aliepoteza ndugu/jamaa yake walisema kwa sauti moja kuwa
” Nia yetu sio kutafuta uchumi bali kuwapa fundisho hawa wakubwa zetu”.
Inasemekana kuwa wakati Bw. Hamad
alipotolewa jela alikowekwa na SMZ (enzi za Rais Salmin Amour) alidai alipwe
TShs milioni ishirini kwa kuwekwa ndani bure.
" Sisi tunadai sio Dollar milioni moja na sio
kwa kile alichokidai Bw Hamad kuwa ni kuwekwa jela bure, bali tunadai kwa
maisha ya jamaa zetu yaliopotezwa bure na ambayo hayawezi kurejeshwa",
walilalamika Wazanzibari hao.
“ Kama kwa kuwekwa ndani bila ya kupoteza
maisha yake Bw. Hamad alidai Milono, je kwa kupotezewa maisha ya
ndugu zetu bure bure tutadai kiasi gani? Bw. Muandishi utalijibu hilo suala
mwenyewe”, walimalizia Wazanzibari hao ambao hawakutaka majina yao yatajwe eti
kwasababu lawsuit bado
haijaenda Mahkama Kuu, Zanzibar.
"Waziri Hamad tokea hapo alikuwa akijipendekezesha
sana kwa wale wenye kumiliki vyombo vya usafiri Visiwani", alieleza jamaa
mmoja, kwa simu yake ambayo ilikuwa ikikatikakatika kila mara. " Vipi
waziri mwezi mmoja nyuma alipoulizwa juu ya meli mpya ya Azam alisema eti kuwa
meli hio haikuletwa kufanya faida bali kusaidia wananchi. Huu ni uwongo na
inaonesha vipi waziri alikuwa anajikomba na wamiliki wa biashara za usafiri
hapa Visiwani".
"Hawa wote ni wanyonyaji na wanajaza
abiria kwenye meli/boti zao kama dagaa na waziri anasema eti nia yao sio kupata
faida." Alieleza huyu Mzanzibari mwenye simu mbovu, huku akionesha hasira
kwenye matamshi yake.
"Ni lazima waziri Hamad afikishwe
kortini kujibu hoja za wananchi, kama sio hivyo mawaziri siku zote watakuwa
wanatumaliza na baadae wanajiuzulu tu" Alinena Mzanzibari mwengine kwenye
simu kutoka nje.
Wachunguzi wa siasa wanasema kama hii class-action
lawsuit
itapelekwa Mahkama Kuu huko Zanzibar basi labda itakuwa ni onyo kwa wale wote
wanaopewa madaraka nchini
Chanzo: Wagagagigikoko News Network ( Wanene)
Hawa jamaa wanataka kumshitaki Hamad Masoud au waziri wa Mawasiliano? Sasa Hamad Masoud anawajibika vipi? Pili niwaulize Hamad Masoud angeweza vipi kudhibiti idadi ya abiria wanaotoka Dar kuja Zanzibar?
ReplyDeleteHawa jamaa wanahitaji kumshitaki mmiliki wa meli na sio Hamad Masoud. Vyenginevyo naona wanajisumbua na kutaka kusumbua watu tu.
Hamad Masoud anahusika kikamilifu na ajali ya Mv Skagit kwakuwa kama waziri ameshindwa kutoa mapendekezo yoyote juu ya udhaifu na kasoro za vyombo viliopo hasa ukitilia maanani kuwa,kuzama kwa mv Skagit hakuhusiani kabisa na wingi wa abiria na mizigo bali ni kutokana na meli yenyewa kutokuwa na muundo unaoruhusu meli hiyo kuelea kwenye bahari ya wazi.akiwa Waziri, baada ya ajali ya mwanzo iliyouwa abiria waliokuwa wakielekea Pemba alitakiwa afanye utafiti wake mwenyewe na achukuwe hatuwa au kama hatua hizo zilikuwa nje ya mamlaka yake basi alilazimika kutowa mapendekezo kwa serkali,Kipenzi chenu Hamad,hakufanya hivyo.kwa hoja hiyo,tunamhesabu kuwa muuwaji kama wauwaji wengine na ni waziri mzembe kama wazembe wengine.
DeleteKwanza, inabidi niwapongeze hawa ndugu zetu wanaoishi nje na ambao waliguswa na huu uzembe wetu hapa ZNZ. Hichi wanachokionesha ni muamko wa aina ya pekee na kama Wazanzibari leo tumefikia kuwa na muamko kama huu basi daima tutasonga mbele. Nimefurahishwa na maneno ya hawa Wazanzibari wa nje waliosema kuwa kujiuzulu sio kujiwajibisha. Haitoshi waziri aliefanya makosa ajiuzulu tu na ndio iwe imekwisha.
ReplyDeleteNd. Anonymous sijui kama unajua chochote kuhusu kile wanachozungumza hawa Wazanzibari wa nje. Ikiwa hujui Hamad Masoud awajibike vipi basi hii ni kweli hujui kitu. Halafu, eti unauliza Hamad Masoud angedhibiti vipi idadi ya watu kwenye boti? Ndugu yangu bora kwanza rejea darasani kabla hujaja kujiaibisha hapa ukumbini. Hivyo unajua kuwa Hamad Masoud alikuwa waziri wa Mawasiliano? Bila ya wasiwasi wowote ule hujui hivyo. Labda unadhania yeye alikuwa mkurugenzi tu!
Ndugu zangu, majibu rasmi naona yametolewa na ndugu zetu waliopo nje. Someni majibu yao hapa:
ReplyDeleteMsimamo wao unatia moyo!