Habari za Punde

Dk Bilal ahutubia kwenye mkutano wa NAM - Tehran Iran

Makamu wa Rais Dk.Mohammed Gharib Bilali akihutubia Mkutano wa Kumi na Sita wa Wakuu wa Nchi za Siasa ya Kutofungamana na Siasa ya Upande wowote  unaomalizika leo  mjini Teheran, Iran. Katika hotuba yake, pamoja na mambo mengine alisisitiza msimamo wa Tanzania kuendelea kupigania haki, kutetea wanyonge, kupinga ubeberu na ukandamizaji  kote duniani, pia aliiasa Jumuiya ya Kimataifa  kutatua migogoro yote kwa njia ya amani.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

1 comment:

  1. acha kusema uwongo dr Bilal , umri wako ni mkubwa karibu utakutana na muumba jee humuogopi? tanzania inaongoza kwa unyanyasaji wa raia na imekuwa inatawala zanzibar kwa mabavu na kuwatumia viongozi kama nyinyi kuendeleza ukoloni , vipi unaisifu serikali ya madhalimu?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.