Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Juma Shamhuna amefanya uteuzi wa wajumbe wanane wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamalaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mwanaidi Abadalla imewataja wajumbe walioteuliwa ni pamoja na Dk. Salim Said Nasser, Sharifa Abeid Salum,Haji Amour Haji na Saleh S.Hamad.
Wengine ni Abadulhamid Idrissa Haji, Radhia Rashid Haroub, Yussuf Khamis Yussuf na Idrissa Muslim Haji.
Katika taarifa yake hiyo, Katibu Mkuu huyo alisema kuwa uteuzi huo umeanza tangu Julai 2 mwaka huu.
IMETOLEWA NA:
IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment