Askari wa Jeshi la Polisi Zanzibar wakiwa na Bendera za Nchi Washiriki katika Mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika wakiwa nje wa Ukumbi wa Mkutano wakisubiri kuwasilisha Bendera kwa utaratibu uliowekwa.
Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mahemmed Gharib Bilal akiwa na Viongozi wa Majeshi ya Polisi wakisimama wakati ukipingwa Wimbo wa Mataifa washiriki katika Mkutano huo.kulia Mkuu wa Jeshi la Polisa Tanzania Said Mwema, Mkuu wa Jeshi la Polisi la Afrika ya Kusini Mangwasashi Victoria, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis, na kushoto Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Silima Perera na Mkuu wa Jeshi la Polisi la Namibia L.T. General Sebastian Ndaitunga.
Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka Nchi za SADC wakisimama kutowa heshima wakati wa kupiga nyimbo za Mataifa washiriki katika Mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka Kusini mwa Afrika uliofanyika katika hoteli ya Zanzibar Beach Mazizini.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akifunguwa Mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika SADC, uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Mazizini Zanzibar.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Silima Perera, akizungumza machake kutoka na Mkutano huo wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi katika ukumbi wa Zanzibar Beach Mazizini Zanzibar.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Said Mwema ambaye ni mwenyeji wa Mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka Kusini mwa Afrika akitowa muktasari wa maandalizi ya Mkutano huo uliofunguliwa na Makamu wa Rais wa Tanzania Dk.Mohammed Gharib Bilal katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Mazizini Zanzibar.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Afrika ya Kusini Magwasashi Victoria akihutubia katika mkutano huo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka nchi mbalimbali za Afrika, wakiwa katika mkutano huo uliofanyika leo Sept 05, 2012 katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar.
Maofisa wa Jeshi la Polisi Tanzania wakifuatilia hutuba ya ufunguzi, kutoka kwa Makamu wa Rais wa Tanzania Dk.Mohammed Gharib Bilal.
Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuufunguwa Mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi wa Nchi za SADC.
No comments:
Post a Comment