TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amemteuwa Dk. Ahmada Hamad Khatib kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kamisheni ya Utalii, Zanzibar.
Kabla ya uteuzi huo Issa Ahmed Othman ndie aliekuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo ambapo sasa amekuwa Mshauri wa Rais wa mambo ya Utalii.
Rais amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu 5(1)(a) cha Sheria ya Kamisheni ya Utalii Namba 7ya 2012
Taarifa iliotolewa na Kaimu Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar Salum Maulid Salum imezidi kueleza kuwa Rais pia amemteuwa Shafi Mussa Haji kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Umeme, Zanzibar.
Kabla ya uteuzi huo Mohamed Hashim Ismail ndie aliekuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo.
DKT Shein amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu 6(1)(a) cha Sheria ya Shirika la Umeme la Zanzibar.
Uteuzi huo unaanza leo tarehe 5/9/2012
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
5/9/2012
KAIMU MKURUGENZI MKUU FCC ATEMBELEA BANDA LA WMA SABASABA
-
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC) Tanzania bi.Hadija Juma
Ngasongwa akisaini kitabu Cha wageni mara baada ya kutembelea banda la
Wakala Wa V...
49 minutes ago
No comments:
Post a Comment