Habari za Punde

Wachina Wakabidhi vifaa vya uchunguzi wa maradhi Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani

 Daktari wa Hospitali ya Abdalla Mzee,  akionesha kifaa cha kukagua maradhi kilichotolewa msaada na China



Serikali ya China imekabidhi vifaa na dawa kwa matumizi ya hospitali ya Abdallah Mzee kisiwa ni Pemba.
 
Akikabidhi vifaa hivo Dr SUN YONG HU kwa uongozi wa spitali hiyo amesema ufadhili huo umekuja kwa ushirikiano uliopo baina ya China na Tanzania.
 
Amesema serikali ya china kwa kuwajali ndugu zao wa Tanzania imeona ni vyema kuwawekea mazingira bora ya afya huku ikiwa ni msukumo wa umoja na undugu unaoendelea baina ya nchi mbili hizo.
 
Akipokea msaada huo Dr dhamana wa spitali hiyo nd ALI JAPE amesema ni jambo la kujivunia kupata ufadhili huo kwani utasaidia kuwanufaisha wakaazi wa pemba na kupelekea kupatikana kwa baadhi ya matibabu ambayo yalikua hayapatikani mpaka mtu asafiri.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.