Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (Troika)
ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) akimpokea Rais Armando Guebuza wa Msumbiji baada ya
kuwasili leo Septemba 3, 2012 katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere jijini Dar es salaam, tayari kwa mkutano wa Troika ya SADC unaotarajiwa
kufanyika kesho Septemba 4, 2012 katika hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency na
kuhudhuriwa na viongozi wa nchi wajumbe wa Asasi hiyo ambao ni Msumbiji ambao
ni Mwenyekiti wa sasa wa SADC, Afrika Kusini aliyekuwa Mwenyekiti wa Asasi hiyo
kabla ya Tanzania, Namibia ambao ni
Makamu Mwenyekiti wa Asasi hiyo ya Troika, pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC) ambao ni wageni waalikwa.
Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (Troika)
ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) akimuonesha Rais Armando Guebuza wa Msumbiji mandhari ya
Bandari ya Dar es salaam kutoka katika
hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency,
baada ya kuwasili leo Septemba 3, 2012
tayari kwa mkutano wa Troika ya SADC unaotarajiwa kufanyika kesho
Septemba 4, 2012 hotelini hapo na kuhudhuriwa na viongozi wa nchi wajumbe wa
Asasi hiyo ambao ni Msumbiji ambao ni Mwenyekiti wa sasa wa SADC, Afrika Kusini
aliyekuwa Mwenyekiti wa Asasi hiyo kabla ya Tanzania, Namibia ambao ni Makamu Mwenyekiti wa Asasi
hiyo ya Troika, pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambao ni
wageni waalikwa.
PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment