Habari za Punde

Dk. Bilal Azinduwa Kampeni za CCM Jimbo la Bububu.

Makamu wa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimnadi Mgombea wa nafasi ya Uwakilishiwa Jimbo la Bububu, Hussein Ibrahim Makungu (BHAA) wakati alipokuwa akizinduaKampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo, uliofanyika kwenye Uwanja wa Geji,mjini Unguja jana
Mbunge wa Iramba Mwigulu Nchemba, akimvisha Skafu yaBendera ya Tanzania, Mgombea wa nafasi ya Uwakilishi wa Jimbo la Bububu,kupitia CCM, Hussein Ibrahim Makungu (BHAA) ikiwa ni ishara ya heshima kuvuautambulisho wake na kumtunuku mgombea huyo,  wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni za uchaguzimdogo wa Jimbo hilo, uliofanyika kwenye Uwanja wa Geji, mjini Unguja jana
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia Wananchi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakati akizinduwa kampeni jimbo la Bububu.
Mbunge wa Iramba na Katibu wa Uchumi na Fedha wa Chama cha Mapinduzi  Mwigulu Nchemba, akitowa sera za CCM, katika mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni Bububu.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, akiwasalimia Wanachama wa CCM katika mkutano wa uzinduzi wa Uchaguzi Mdogo wa jimbo la Bububu. 
Makamu wa Pili wa Ris wa Zanzibar na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Balozi Seif Ali Iddi, akiwasalimia Wananchi wa jimbo la Bububu wakati wa uzinduzi wa kampeni.


Mashabiki na wanachama wa CCM, wakishangiliana kufurahia hotuba ya Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi hao kwenye shereheza uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo, uliofanyika kwenyeUwanja wa Geji, mjini Unguja
 Viongozi wakipata burudani ikitolewa na Msanii wa Kikundi cha Jahazi Mzee Yussuf.
 Ayeya ndivyo inavyoonekana msanii huyu Mzee Yussuf akitowa burudani kwa wapenzi wake katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni ya Chama cha Mapinduzi.
 Mwakilishi Mtarajiwa wa Jimbo la Bububu Hussein Ibrahim BHAA na Mbungev wa jimbo hilo Sururu, wakienda kumtunza msanii Mzee Yussuf, akitowa burudani katika uzinduzi wa Kampeni.
 Hivi ndivyo ilivyokuwa katika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Mapinduzi.
 Wanachama wa Cham cha Mapinduzi  wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Tanzania  na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizindua Kampeni za Chama cha Mapinduzi kwa Mgombea wake wa Jimbo la Bububu. 

 Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wakishangiria Sera za Chama chao wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za CCM.
 Msanii Mzee Yussuf, akitowa burudani kwa Wanachama wa Chama cha Mapinduzi katika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Bububu zilizofanyika katika uwanja wa Kwa Geji Kijichi Bububu. 

2 comments:

  1. Mzee Mapara,

    Kwa kweli nahisi umeonesha upendeleo ulipowatambulisha wagombea wa uwakilishi wa jimbo la Bububu. Mgombea wa CCM umemtambulisha kama "mwakilishi mtarajiwa" wakati yule wa CUF umemwita mgombea tu.Hata ulivyoielezea ile caption pia kuna tofauti. Kwa kweli hii blog ni yako na sisi ni waangaliaji tu. Lakini nahisi wewe ulihitaji kuuweka kando upenzi wako kama mwandishi.

    ReplyDelete
  2. Kwa kuongezea tu na mimi narejea kauli hiyo hiyo ya kumtambulisha Bhaa kama "MWAKILISHI MTARAJIWA" kauli hii si ya kusemwa na mwandishi bali na makada wa chama, ikibidi mwandishi kuitumia kauli hii basi itumike kwa wagombea wote. Na zaidi bwana Mapara ameweka picha 17 za kampeni za CCM, wakati ameweka picha 8 tu kwa chama cha CUF. Wataalamu wanasema picha inasema mara 1000 kuliko maandishi. Hivyo ni kusema tu kwa kuanzia "uwanja ulio sawa" haujapatikana katika blog ya "zanzinews" ambapo sisi tunaitumiasana kwa kupata habari za nyumbani.
    Bwana Mapara jipange vizuri kimaadili ya kazi.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.