Habari za Punde

Maalim Seif mgeni rasmi maadhimisho ya miaka 10 ya tiba asilia


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akishuhudia kazi ya ukanzi "massage" katika maadhimisho ya kumi ya tiba asilia barani Afrika yalivyofanyika Victoria garden Zanzibar.

Dr. Jon IL Gu kutoka Korea akitoa maelezo juu ya matumizi ya dawa asilia, aliposhiriki kwenye maonyesho ya dawa hizo, ikiwa ni maadhimisho ya miaka 10 ya tiba asilia barani Afrika. Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad (wa tatu kushoto).

Mwenyekiti wa Baraza la tiba asilia Zanzibar Bi Mayasa Ali akielezea mafanikio ya baraza hilo tangu kuanzishwa kwake, kwenye maadhimisho ya miaka kumi ya tiba asilia barani Afrika yaliyofanyika bustani ya Victoria, mjini Zanzibar.


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiangalia dawa za miti shamba katika maadhimisho ya kumi ya tiba asilia barani Afrika yalivyofanyika Victoria garden Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.