Na
Haroub Hussein
MABINGWA
watetezi wa ligi kuu ya soka Zanzibar
timu ya Super Falcon, wataanza kampeni za kulibakisha taji lao kwa kupambana na
Chipukizi katika uwanja wa Gombani.
Katika
ligi kuu msimu ujao inayotarajiwa kuanza Septemba 8 chini ya udhamini wa
kinywaji cha Grand Malt, makamu bingwa Jamhuri atakuwa na kibarua dhidi ya
wanamaji wa KMKM katika uwanja wa Amaan.
Kwa
mujibu wa ratiba iliyotolewa na Chama cha Soka Zanzibar
(ZFA), Jumapili ya Septemba 9, masarahange wa Malindi na wavuta nanga wa
Bandari, watatiana mikononi uwanja wa Amaan, huku wajenga uchumi wa Duma,
wakivutana na Jamhuri huko Gombani Pemba .
Septemba
10 kutakuwa na mchezo mmoja tu, ambapo nyasi za Amaan zitakuwa mashakani
kuhimili madaluga ya timu za Mtende na Zimamoto, na mzunguko wa kwanza
utamalizika Septemba 11 kwa mechi kati ya Mundu na Chuoni.
Mechi
zote hizo zimepangwa kuanza wakati wa saa kumi.
Ligi
hiyo itakuwa mapumzikoni kwa siku tatu, ikitarajiwa kurudi viwanjani Septemba
15, kwa mechi kati ya KMKM na Malindi uwanja wa Amaan, na Super Falcon na Duma,
katika dimba la Gombani.
No comments:
Post a Comment