Habari za Punde

Ligi Daraja la Kwanza Taifa Kipanga na Polisi imeshinda 3--0

 Timu za Vikosi zina wapenzi wengi kuliko timu za Uraiani na kuvuta watu wengi wakati zinapicheza, kama inavyoonekana wakati wa mchezo wa Ligi ya Taifa daraja la kwanza kati ya timu ya Kipanga na Polisi zikiwania kupanda daraja la Ligi Kuu ya Zanzibar mwakani.



 Mshambuliaji wa timu ya Kipanga akipiga kichwa golini kwa timu ya Polisi lakini kichwa hicho hakikuleta madhara golini.
 Golikipa wa Timu ya Kipanga akiokoa mpira na huko mshambuliaji wa timu ya Polisi akijaribu kumzuia mchezaji huyo,
 Mchezaji wa timu ya Kipanga akimiliki mpira katika mchezo wa ligi ya taifa daraja la kwanza uliofanyika uwanja wa Mao, timu ya Polisi imeshinda 3-0 
 Mashabiki wa timu ya Pilosi wakicheza bwaride wakipita katika benchi la timu ya Kipanga baada ya mchezo kumalizika timu ya Polisi ikitoka kivua mbele kwa ushindi wa mabao 3--0, mchezo uliofanyika uwanja wa Mao.
Hivi ndivyo ulivyokuwa wakati wa mchezo wa upin zani wa ligi daraja la kwanza taifa Zanzibar zikiwania kupanda daraja.
 
Uwanja ukiwa umejaa ikionesha timu za Vikosi zina Wapenzi wengi ndio maana hali ikiwa hivi katika uwanja wa Mao ikikumbusha siku za timu za Small Simba ( Moto Small), Malindi na nyeginezo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.