Habari za Punde

Balozi Seif amjuulia hali Naibu Waziri wa elimu na mafunzo ya amali Mh Zahra Ali Hamadi

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mkuu wa shughuli za Serikali Balozi Seif Ali Iddi akimjuilia hali Mwakilishi wa Viti Maamu CUF ambae pia ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar { wema } Mh. Zahra Ali Hamadi akiwa mapumzikoni nyumbani kwake Mombasa Mbuyu mnene baada ya ushauri wa Daktari wa kutakiwa apumzike kutokana na afya yake.
Nyuma yao ni Baba Mzazi wa Mheshimiwa Zahra Mzee Ali Hamad.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh. Zahra Ali Hamadi akimuelezea maendeleo ya afya yake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliyefika kumkagua nyumbani kwake Mombasa Mbuyu mnene.

2 comments:

  1. Hii inapendeza sana. Zanzibar tumetoka mbali. Inshallah Mungu atujaalie tuendelee kupendana hivi hivi bila kubaguana kwa itikadi za kisiasa.

    ReplyDelete
  2. Amin, itikadi za siasa zisiwe sababu ya kupoteza utu wetu.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.